Date: 
03-06-2021
Reading: 
Matendo 15:6-11 (Acts 15:6-11)

ALHAMISI TAREHE 3 JUNI 2021, ASUBUHI

Matendo ya Mitume 15:6-11

6 Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo.
7 Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.
8 Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi;
9 wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.
10 Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua.
11 Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.

Mungu mmoja;

Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Wakiwa Antiokia, Paulo na Barnaba wanahubiri, lakini baadhi ya mafundisho yao yanakataliwa. Ndipo ikaamuliwa waende Yerusalemu, na katika ibada, Petro ndipo anakuja na ujumbe tuliousoma.

Petro anaeleza Mungu alivyowachagua, akawaongoza kuhubiri kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, akiwaasa kutotawaliwa na mawazo yao, bali neno la Mungu.

Petro anamalizia kuwa wokovu ni kwa neema ya Mungu. Huu ndiyo ujumbe wangu kwako asubuhi hii, kwamba Mungu ametuchagua tumtumikie, tukiutangaza ufalme wake, kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Tudumu katika utume huu, ili Kanisa lake litawaliwe na neno lake, na siyo mawazo yetu.

Siku njema.


THURSDAY 3RD JUNE 2021, MORNING

Acts 15:6-11

The apostles and elders met to consider this question. After much discussion, Peter got up and addressed them: “Brothers, you know that some time ago God made a choice among you that the Gentiles might hear from my lips the message of the gospel and believe. God, who knows the heart, showed that he accepted them by giving the Holy Spirit to them, just as he did to us. He did not discriminate between us and them, for he purified their hearts by faith. 10 Now then, why do you try to test God by putting on the necks of Gentiles a yoke that neither we nor our ancestors have been able to bear? 11 No! We believe it is through the grace of our Lord Jesus that we are saved, just as they are.”

Read full chapter

One God;

Father, Son and Holy Spirit;

In Antioch, Paul and Barnabas preach, but some of their teachings are rejected. Then it was decided to go to Jerusalem, and in worship, Peter then came with the message we read.

Peter explains how God chose them, led them to preach by the power of the Holy Spirit, exhorting them not to be ruled by their own ideas, but by the word of God.

Peter concludes that salvation is by God's grace. This is my message to you this morning, that God has chosen us to serve, proclaiming his kingdom, with the help of the Holy Spirit. Let us abide in this mission, that his Church may be governed by his word, and not our thoughts.