Date: 
10-04-2021
Reading: 
Matendo 13:34-40

Jumamosi tarehe 10 Aprili 2021 asubuhi 

Matendo ya Mitume 13:34-40

[34]Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi, 

Nitawapa ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini.

[35]Kwa hiyo anena na pengine, 

Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu.

[36]Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.

[37]Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona uharibifu.

[38]Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi;

[39]na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.

[40]Angalieni, basi, isiwajilie habari ile iliyonenwa katika manabii.

Yesu ameshinda kifo;

Mtume Paulo bado yupo Antiokia akifafanua habari za Yesu. Katika somo la leo asubuhi, anakazia kuwa kwa njia ya ufufuo wa Bwana Yesu, tunahubiriwa msamaha wa dhambi. Na kila amwaminiye huhesabiwa haki.

Sisi hatuna shaka, hivyo ni habari ya kweli kuwa Yesu alifufuka, na anatutangazia msamaha wa dhambi. Wajibu wetu ni kumwamini, ili tuhesabiwe haki.

Jumamosi njema.