MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 04 DESEMBA, 2022    

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

BWANA ANAKUJA KATIKA UTUKUFU WAKE

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 27/11/22

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wakumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. AlhamisiMaombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Kanisa Kuu Azania Front limepanga kuadhimisha uimbaji wa Nyimbo za Krismas (Christmas Carols) Jumamosi ya tarehe 17 Desemba, 2022 kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 1:00 usiku. Kwaya zetu zote zinazohudumu katika ibada zetu zote hapa Kanisa Kuu, zitahusika. Nyimbo zitakazopewa kipaumbele ni zile za Kristmas kutoka katika kitabu chetu cha Tumwabudu Mungu Wetu (TMW). Maelekezo kuhusu matayarisho hayo tayari viongozi wa vikundi wanayo. Tusiache kuiombea siku hiyo ifanikiwe.Wote tunakaribishwa kuhudhuria. Mungu awabariki sana.

6. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwashukuru Wanawake wote waliohudhuria maadhimisho ya Krismasi Kidayosisi yaliyofanyika jana jumamosi tarehe 03/12/2022 Usharika wa Boko. Mungu awabariki sana.

7. Uongozi wa Kwaya Kuu ya Usharika unapenda kuwaomba Wanakwaya wa vikundi vyote kushiriki na kuungana nao kwenye ibada ya Christmas Carols itakayofanyika siku ya ijumaa tarehe 23/12/2022 saa 11.00 jioni Kanisa la St Alban’s Anglican Cathedral. Mazoezi yataanza siku ya jumanne tarehe 06/12/2022 saa 11.00 jioni. Mungu awawezeshe kufika kwenye mazoezi na kwa wakati.

8. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 17/12/2022. NDOA HII ITAFUNGWA USHARIKA WA KKKT NKOARANGA DAYOSISI YA MERU KATI YA

Bw. Urasa Olufemi Sarakikya na Bi. Gloria Nduminsary Swai

PIA NDO HII IFUATAYO ITAFUNGWA USHARIKA WA KKKT NGAYA MOSHI KATI YA 

Bw. Elifuraha Israel lema na Bi. Victoria Benny Sifael

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 10/12/2022

SAA 9.00 ALASIRI  

Bw. Raphael Joseph Sakita na Bi. Tasiana Cyprian Massimba

NDOA HII IFUATAYO ITAFUNGWA PAROKIA YA TEGETA KATI YA

Bw. Emmanuel Olotu na Bi. Edna Sikujua  

9. NYUMBA KWA NYUMBA 

  • Masaki na Oyserbay: kwa Bwana na Bibi Sepi Mawalla.
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na BIbi Mcharo Mlaki
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Happiness Nkya. Alykhan Rd Plot 256

10. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.