MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 31 JULAI, 2022

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

MUNGU AMEJAA NEEMA INAYOTUWEZESHA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti. 

3. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Leo tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.

6. Leo kila msharika atatoa mapendekezo ya majina ya wanaofaa kuwa Wazee wa Kanisa. Tujiandae kwa kutoa mapendekezo hayo. 

7. Jumapili ijayo tarehe 07/08/2022 tutamtolea Mungu fungu la Kumi. Washarika tujiandae.

8. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

Kwa mara ya Kwanza tunatangaza Ndoa zitakazofungwa tarehe 20/08/2022 

SAA 09:00 ALASIRI

Bw. John Ezekiel Mfugale na Bi. Tumaini Herico

Kwa mara ya Tatu tunatangaza Ndoa zitakazofungwa tarehe 06/08/2022 

SAA 08:00 MCHANA

Dr. Zephania Dick Peter Gega na Dr. Lilian Willy Mbise

Matangazo mengine ya Ndoa yapo kwenye ubao wa Matangazo.

9. NYUMBA KWA NYUMBA

  • Masaki na Oyserbay: Kwa Bwana Abdiel Mengi
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Korosso
  • Mjini kati: watafanya kwa njia ya Mtandao.
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
  • Kinondoni: Watatangaziana
  • Upanga:Kwa Bwana na Bibi Mathew J. Munisi- Alykhan Road 

10. Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki