MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 24 APRIL, 2022

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI KRISTO AJIFUNUA KWETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti. 

3. Matoleo ya Tarehe 17/04/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Uongozi wa Shule ya Jumapili unapenda kuwaomba Wazazi kuwaruhusu watoto kuja kwenye mazoezi ya kujifunza nyimbo kwa ajili ya tamasha la uimbaji Kijimbo. Mazoezi ni kuanzia saa 8.00 mchana kila jumamosi.

6. Uongozi wa Umoja wa Wanawake wakishirikiana na Uongozi wa Usharika umeandaa semina ya Neno la Mungu na ujasiliamali. Semina hiyo itafanyika jumamosi ijayo tarehe 30/04/2022 katika kituo cha Kiroho cha Consolata kilichopo Bunju Dar es Salaam. Safari ya kuelekea huko itaanzia hapa Usharikani 1.00 asubuhi, Wanawake wote mfike mapema bila kuchelewa.

7. SHUKRANI ZA TAREHE 01/05/2022

IBADA YA KWANZA

- Kwaya ya Agape watamshukuru Mungu kwa kuwawezesha kutoa huduma kwa wahitaji katika Hospitali ya Muhimbili kwa miaka minne, kutoa Video ya Kwaya pamoja na Baraka nyingi Ndoa, Elimu na Watoto.

Neno: Zaburi 112: 5-6, Zaburi 111:1-5, Wimbo:Mungu ee Mungu (Kwaya ya Agape)

- Familia ya Marehemu Franklin Mkony watamshukuru Mungu kwa ulinzi na faraja tangu Baba yao mpendwa alipotwaliwa miaka 4 iliyopita. 

Neno: Zaburi 23, Wimbo: TMW 424, Ninawaza habari (Kwaya ya Upendo)

8. NYUMBA KWA NYUMBA

- Masaki na Oyserbay: Kwa Prof. na Bibi Mashala

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe

- Mjini kati: watafanya njia ya Mtandao.

- Kinondoni: Kwa Prof. na Bibi S. Kulaba

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bw. Yono na Bi Scholastica Kevel

9. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZITAKAZOFUNGWA TAREHE 30/04/2022  

SAA 9.00 ALASIRI

- Bw. Heri Willy Mwakisole na Bi. Rehema Ismaily Mohamed

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo.

10. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.