MATANGAZO YA USHARIKA

 LEO TAREHE 20 NOVEMBA, 2022    

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

UZIMA WA ULIMWENGU UJAO

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 13/11/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. AlhamisiMaombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwashukuru Wazazi wote waliowahimiza watoto kuhudhuria kwenye mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa Mwaka wa Kwanza na wa Pili na wale waliopata Kyaliyofanyika jana jumamosi tarehe 19/11/2022 kuanzia saa 2.30 asubuhi hapa Usharikani.  

6. Uongozi wa Umoja wa wanawake unapenda kuwashukuru wanawake wote waliohudhuria ibada ya Maadhimisho ya Krismas yaliyofanyika jana jumamosi tarehe 19/11/2022 saa 3.00 asubuhi katika Usharika wa Mwanagati. Mungu awabariki

7. Umoja wa Vijana unapenda kuwatangazia vijana wote na Washarika wote kuwa kutakuwa na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya igizo la Krismasi. Mazoezi yatafanyika kila siku ya jumatatu saa 11.00 jioni na Jumamosi saa 10.00 jioni. Wote mnakaribishwa.

8. Kanisa Kuu Azania Front limepanga kuadhimisha uimbaji wa Nyimbo za Krismas (Christmas Carols) Jumamosi ya tarehe 17 Desemba, 2022 kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 1:00 usiku. Kwaya zetu zote zinazohudumu katika ibada zetu zote hapa Kanisa Kuu, zitahusika. Nyimbo zitakazopewa kipaumbele ni zile za Kristmas kutoka katika kitabu chetu cha Tumwabudu Mungu Wetu (TMW). Maelekezo kuhusu matayarisho hayo tayari viongozi wa vikundi wanayo. Tusiache kuiombea siku hiyo ifanikiwe.Wote tunakaribishwa kuhudhuria. Mungu awabariki sana.

9. Jumamosi ijayo tarehe 26/11/2022 ni Siku ya Ubarikio wa watoto wa Kipaimara kwa ibada ya Kiswahili. Hivyo Jumatano ijayo tarehe 23/11/222 ni siku ya kupima ufahamu wanafunzi wa Kipaimara. Uongozi wa Usharika unawaomba wazazi na Wadhamini pamoja na watoto kufika Kanisani saa kumi kamili jioni. Mnaombwa sana kuzingatia kufika kwa wakati.

10. Jumapili ijayo tarehe 27/11/222 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.

11. Mkutano Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) utaanza Jumapili ijayo tarehe 27/11/2022 katika Usharika wa KKKT Mbezi Beach. Washarika tuuombee Mkutano huu muhimu.

12. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 26/11/2022 AMBAYO ITAFUNGWA ST. JOSEPH KATI YA

Bw. Clement Makagabila na Bi. Lora-Ester Brown Foi

    

TAREHE 27/11/2022

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Joel Rutashobya na Bi. Annamaria Patrick

Matangazo mengine yapo kwenye ubao wa Matangazo.

13.  NYUMBA KWA NYUMBA 

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Raymond Sangiwa

- Kinondoni: Kwa Eng. na Bibi Danford Mariki

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach:Kwa Bwana na Bibi Robby Monyo saa 12 jioni.

14. [ Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azaniafront.org, pia tupo Facebook na Instagram.]

15. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.