MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 18 SEPTEMBA, 2022

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

UWAKILI WETU KWA MUNGU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti. Matoleo ya Tarehe 11/09/2022   

3. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Jumapili ijayo tarehe 25/09/2022 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae

6. Mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya Reformation yanaendelea kila siku ya JUMANNE, JUMATANO na IJUMAA Saa 11.00 jioni tafadhali waimbaji wote mnaombwa kuhudhuria na kufika kwa wakati. 

7. Jumapili ijayo tarehe 25/09/2022 katika ibada ya kwanza saa 1.00 asubuhi familia ya Mwalimu Amri Hingi watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea. Pia binti yake Diana kuongeza mwaka, siku yake ya kuzaliwa. 

 Neno: Zaburi 145:1-10, Wimbo: Yesu nakupenda toka Kwaya ya Agape 

8. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 08/10/2022

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Baraka Mbangile na Bi. Winfrida msabuni

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 24/09/2022

SAA 5.00 ASUBUHI

Bw. Daniel William Baumba na Bi. Wellu Samwel Sira

NDOA IFUATAYO ITAFUNGWA KKKT USHARIKA WA CHAMWINO MOROGORO KATI YA 

Bw. Winfred w. Ngullo na Bi. Ireen Joel matimbwi    

Matangazo mengine ya Ndoa yapo kwenye ubao wa Matangazo.

9. NYUMBA KWA NYUMBA 

  • Masaki na Oyserbay: Kwa Bwana na Bibi David Mollel
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa
  • Mjini kati: Kwa Mama Omega Mongi.
  •  
  • Kinondoni: Kwa Eng. Na Bibi Danford Mariki    
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Dr. Abedi na Eng. Kinasha
  • Upanga: Kwa Susana Mboya        
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Lasway

10. Zamu: Zamu za wazee ni kundi laPili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.