MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 17 JULAI, 2022

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

TUNAITWA KUWA WANAFUNZI NA WAFUASI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: wageni waliotufikia na vyeti ni (1) Angetile Mwakang’ata toka Kanisa la Moravian Tanzania Usharika wa Jacaranda Mbeya, anakuja kwenye matibabu.(2) Dorah Brown Chanafi toka Usharika wa Kunduchi anahamia hapa. Matoleo ya Tarehe 10/07/2022 

3. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. SHUKRANI

Jumapili ijayo tarehe 24/07/2022 katika ibada ya kwanza saa 1.00 asubuhi familia ya Bwana na Bibi timon Msangi watamshukuru Mungu kwa Mzee Timon kufikisha miaka 83.

Neno: Zaburi 71:15-19, Wimbo: TMW 295

6. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

Kwa mara ya Kwanza tunatangaza Ndoa zitakazofungwa tarehe 06/08/2022 

SAA 08:00 MCHANA

  • Dr. Zephania Dick Peter Gega na Dr. Lilian Willy Mbise

Kwa mara ya Tatu tunatangaza Ndoa zitakazofungwa tarehe 23/07/2022 

SAA 10:00 JIONI

  • Bw. Raymond Mathew Munisi na Bi. Doris Elishilia Sindila

Matangazo mengine ya Ndoa yapo kwenye ubao wa Matangazo.

7. NYUMBA KWA NYUMBA

  • Masaki na Oyserbay: Kwa Mzee Elipina Mlaki
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Raymond Sangiwa
  • Mjini kati: watafanya kwa njia ya Mtandao.
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
  • Kinondoni: Kwa Prof G. Mmari
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Laurance Mlaki
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Happiness Nkya
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Watatangaziana

8. Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki