MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 16 OKTOBA, 2022    

NENO LINALOTUONGOZA NI

UPENDO WA KWELI WATOKA KWA MUNGU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 09/10/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. AlhamisiMaombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia kuwa mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa Mwaka wa Kwanza na wa Pili yatafanyika tarehe 19/11/2022 kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana hapa Usharikani. Wale waliopata Kipaimara wenye umri wa miaka 15 pia wanakaribishwa kwenye mafundisho haya. Wazazi na Walezi mnaombwa kuandikisha watoto watakaohudhuria kwa Parish Worker ili kufanya maandalizi haya.

6. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 05/11/2022  

SAA 6.00 MCHANA

Bw. Victor Frank Koyanga na Bi. Annansia Godbless Uronu

Matangazo mengine yapo kwenye ubao wa Matangazo.

7. NYUMBA KWA NYUMBA 

- Masaki na Oyserbay: kwa Bwana na Bibi Witson Moshi.

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lymo

- Mjini kati: watatangaziana

- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Rweikiza

- Kinondoni: Kwa Prof. G. Mmari    

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Watatangaziana

- Upanga: Watatangaziana.

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Robnson Monyo 

8. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili  

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu Mungu ayabariki.