MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 12 JUNI, 2022
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
UTATU MTAKATIFU MUNGU MMOJA; BABA, MWANA, NA ROHO MTAKATIFU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.
3. Matoleo ya Tarehe 05/06/2022
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.
5. Jumapili ijayo Tarehe 18/06/2022 kutakuwa na tamasha la watoto Jimbo la Kati, hivyo wazazi mnaombwa kuwaleta watoto hapa Kanisani mapema saa 12.30 asubuhi kwa ajili ya kwenda huko kwenye Tamasha hili.
6. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia washarika wote kuwa mnamo tarehe 25/06/2022 kutakuwa na kambi ya upimaji wa Afya hapa Kanisani Azania Front. Upimaji huu utakuwa wa bure. Kambi hii itakuwa na zaidi ya vituo kumi kwa magonjwa mbali mbali. Upimaji huu umelenga zaidi kwa Washarika wetu. Hivyo kamati inaomba washarika wajitayarishe na kujitokeza siku hiyo. Aidha kwa sababu ya uwingi wa vituo vya upimaji gharama zitakuwa kubwa hivyo yeyote atakayependa kuchangia anaweza kuwaona wanakamati, Parish Worker au Mhasibu wa Usharika. Kamati inaomba pia kuiombea siku hiyo.
7. Tunapenda kuwataarifu kuwa Mkutano Mkuu wa wanahisa wa Maendeleo Bank utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni, 2022 katika ukumbi wa Msasani Tower, Dar es Salaam kuanzia saa (nne) 4:00 asubuhi. Pia Mkutano huu utafanyika kwa njia ya mtandao Zoom na anuani ya mkutano itatumwa kwenye barua pepe au namba ya simu ya Mwanahisa iliyosajiliwa Benki. Wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria
8. Familia ya Bwana na Bibi Moses Kombe wamepata zawadi ya mtoto wa kike. Mama, Baba na mtoto wanaendelea vizuri.
9. Uongozi wa Wajane na Wagane wanatoa shukrani nyingi kwa Uongozi wa Usharika Mch. Kiongozi, Baraza la Wazee na Washarika wote kwa kutuwezesha kwenda kufanya Semina katika Mtaa wetu wa Tabora jumamosi iliyopita tarehe 04/06/2022. Semina ilikuwa nzuri sana. Mungu awabariki.
10. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 17/06/2022 KATI YA
Bw. Aidan Magnus Large na Bi. Hilda Martin Kasyanju
Matangazo mengine ya Ndoa yapo kwenye ubao wa Matangazo.
11. Jumamosi ijayo tarehe 18/06/2022 kutakuwa na Kongamano la vijana wa kiume litakalofanyika Usharika wa Ubungo kuanzia saa 2.30 asubuhi. Vijana wote wa kiume mnaombwa kujiandaa na kufika kwenye Kongamano hili muhimu.
12. NYUMBA KWA NYUMBA
Masaki na Oyserbay: Kwa Bwana na Bibi Kimweri
Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Matee
Mjini kati: watafanya njia ya Mtandao.
Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki
Teta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Buchanagandi
Upanga: Kwa Bwana na Bibi Kavugha. Mt. Mazengo PC Na. 18
13. Ratiba ya Uchaguzi: Leo Usharika utapokea mapendekezo ya Majina 15 ya waalimu wa Shule ya Jumapili wanaofaa kuongoza. Majina 25 ya Umoja wa Wanawake, Majina 25 ya Vijana na Majina 25 ya Wanaume.
14. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Kwanza.
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.