MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 01 OKTOBA, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI TUWAPENDE WATOTO WETU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Kamati ya Missioni na Uinjilisti inawaarifu washarika wote kuwa ile semina ya maisha ya maombi iliyoanza Jumatatu tarehe 25/09/2017 inakamili leo tarehe 01.10.2017 10.30 jioni. Semina hiyo inayofundishwa na Mchungaji Deogratius Msanya toka KKKT Moshi imefundisha mambo mazuri kuhusu maisha ya maombi kwa Mkristo na jinsi yanavyoweza kutuunganisha na Mungu katika kila nyanja ya maisha.  Washarika mnakaribishwa kushiriki katika somo hili muhimu.  Na leo tutatoa sadaka ya shukrani kwa neema tuliyopata juu ya semina hii.  Wote mnakaribishwa.  Aidha Alhamisi ijayo tarehe 05/10/2017 saa 11.30 jioni tutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi na somo kuu itasimamia EZRA 9. Mnenaji atakuwa ni  Emmanuel Frank wa KKKT Tumbi. Wote mnakaribishwa.

4. Leo  ni sikukuu ya Mikaeli na Watoto.

5. Vitenge vya Miaka mia tano ya matengenezo ya Kanisa vipo.  Vitauzwa hapo nje na viongozi wa Umoja wa Wanawake kwa bei ya sh. 15,000/=.  Aidha Vitenge vya Kiharaka navyo bado vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya shilingi elf 10.  Washarika karibuni.

6. Jumapili ijayo tarehe 08/10/2017 Mzee Evatt Kuzilwa pamoja na familia watamtolea Mungu shukrani ya pekee kwa ulinzi wake tangu mke wake mpendwa alipotwaliwa na Bwana mwaka mmoja uliopita.

Neno: Zaburi 105:1-5, Wimbo:TMW 318, Kwaya ya Kuu (Yesu mwokozi Yu Mlinzi wangu)

7. Jumapili ijayo tarehe 08/10/2017 tutamtolea Mungu fungu la kumi.  Washarika tujiandae. Aidha siku hiyo tarehe 08/10/2017 ni siku ya ubatizo wa watoto wadogo na kurudi kundini.  Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

8.Tunapenda kuwatangazia washarika wote kuwa mafundisho ya ndoa za mwezi wa Oktoba, Novemba, Disemba na Januari 2018 yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

9. Jumanne ijayo tarehe 03/10/2017 kutakuwa na kikao cha Baraza la Wazee.

 

10. NDOA

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

11. TANZIA

Usharika unasikitika kutangaza kifo cha msharika muimbaji wa Kwaya Kuu, Kinamama, Upendo, vijana na Kwaya ya Umoja Mama Tabu Ndziku, kilichotokea siku ya Jumanne tarehe 26.09.2017 kwa ajali na kuzikwa tarehe 29.09.201 Ilula Iringa. Picha yake imebandikwa kwenye ubao wa matangazo na kwenye milango. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe..

 

12. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: kwa Bwana na Bibi Cuthbet swai
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Itemba
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi T. Msangi
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi D. Mollel
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo:  Kwa Mzee E. Kuzilwa
  • Mjini kati: Kwa Bibi Angela Malyi
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:Kwa Bwana na Bibi Frank Korassa

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili Watashirikiana na watoto

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.