MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 06 OCTOBA, 2019

 

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

MUNGU HUTUTUNZA KWA UWEZO WAKE MKUU.

 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyefika na Cheti. Kama kuna wageni ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.

3. Matoleo ya Tarehe 29/09/2019

4. Alhamisi ijayo tarehe 10/10/2019 saa 11.00 jioni kutakuwa na kipindi  cha maombi na maombezi hapa usharikani.  Wote mnakaribishwa.

5. Tunapenda kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu siku za juma hapa Usharikani, Morning Glory inayoanza saa 12.00 – 1.00 asubuhi, siku ya Jumatatu hadi Ijumaa,  ambayo hukupa fursa ya kuanza kazi na uwepo wa Mungu.  Ibada ya Mchana kila siku saa 7.00 – 7.30 mchana ambayo inakupa nafasi ya kupata faragha  binafsi na Mungu.  Wote mnakaribishwa.

6. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia washarika wote kuwa mafundisho ya Elimu ya Afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa mwaka huu yatafanyika tarehe 26/10/2019 kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.  Mafundisho haya yatawajumuisha pia wazazi wa watoto hawa na vile vile waliopata Kipaimara kwa miaka ya hivi karibuni na walio na umri hadi miaka 15.  Tunaomba wanafunzi na wazazi watakaoshiriki mafundisho hayo wajiandikishe kwa Parish Worker au kwa katibu wa Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii Dr. Lilian Mbowe.

7. Leo tarehe 06/10/2019 ni jumapili ya kwanza ya mwezi, na siku ambayo tunaikaribia madhabahu ya Bwana na zaka zetu, yaani sehemu ya kumi ya mapato yetu ya ajira  na biashara zetu.  Kumbuka iwe zaka kamili, ili iwe takatifu na ya kumpendeza Bwana.  Aidha ni siku pia tunayoikabili madhabahu ya Mungu kwa dua, sala na maombi kwa ajili yetu binafsi, famila zetu, Kanisa letu, nchi na serikali yetu, ili Mungu atutangulie na kutuongoza katika yote kwa mwezi Octoba. 

8. Umoja wa Wanawake Azania Front wanapenda kutangazia kuwa kutakuwa na kikombe cha chai na Baba Askofu tarehe 18/10/2019 saa 10.30 jioni Usharika wa KKKT Ubungo. Madhumuni ya kikombe hiki cha chai ni kuchangisha fedha kwa ajili ya ununuzi wa vitanda na vifaa kwa ajili ya Wodi ya Wanawake Mjawa Hospitali.  Wote mnakaribishwa kadi ziko kwa viongozi wa Wanawake na kwa Parish Worker.

9. Kamati ya Malezi pamoja na Uongozi wa Shule ya Jumapili unapenda kuwashukuru sana washarika kwa kufanikisha sikukuu ya Michael na watoto iliyofanyika jumapili iliyopita tarehe 29/09/2019. Michango hilyo ilikuwa ni kiasi cha shilingi 10,150,000. Mungu awabariki.

10. Familia ya Bwana na Bibi Colex Mbise wamepata zawadi ya mtoto wa kike tarehe 01/10/2019 katika hospitali ya Palestina Sinza. Baba, Mama na Mtoto wanaendelea vizuri.

11. Jumapili ijayo tarehe 13/10/2019 ni siku ya ubatizo na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

12. NDOA

HAKUNA NDOA ZA WASHARIKA

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.Karibu na duka letu la vitabu.

11. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Wazo/Tegeta/Kunduchi/Bahari Beach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Laurance Mlaki
  • Mwenge/Kijitonyama/Makumbusho/Sinza/Ubungo/Makongo: Kwa Mama Mamkwe
  • Mjini kati: Watatangaziana
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: …………………………..
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Henry Mwanyika
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Kimweri
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mathias Kavugha
  • Kinondoni: Kwa Profes G. Mmari
  • Tabata: ………………………………………………

13. Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki. 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

IBADA YA I

Mzee  N. Buchanagandi         - Neno: Zab. 37:29-38 Yer. 39:15-18 Mt. 14:29-36

Mzee  M. Mwakilembe            - Matangazo   

Mzee  Beatrice Bomani         - Sunday School

Mzee  Samuel Swai               - Ndoa   

 

IBADA YA II

Mzee  Tulizo Sanga               - Neno:  Zab. 37:29-38 Yer. 39:15-18 Mt. 14:29-36

Mzee  Theophilus Mlaki          - Matangazo

Mzee Judica A. Lawson         - Sunday School

Mzee Zebadia Moshi             - Ndoa