MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 04 AGOSTI, 2019

 

SIKU YA BWANA YA 7 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

NEEMA YA MUNGU YATUWEZESHA KUZAA MATUNDA MEMA

 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyefika.

3. Alhamisi ijayo tarehe 08/08/2019 saa 10.00 jioni tutakuwana kipindicha maombi na maombezi yatakayoongozwa na Mwl. Munisaria Swai toka KKKT Kurasini.Karibuni Wote.

4. Tunapenda kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu siku za juma hapa Usharikani, Morning Glory inayoanza saa 12.00 – 1.00 asubuhi, siku ya Jumatatu hadi Ijumaa,ambayo hukupa fursa ya kuanza kazi na uwepo wa Mungu.Ibada ya Mchana kila siku saa 7.00 – 7.30 mchana ambayo inakupa nafasi ya kupata faraghabinafsi na Mungu.Wote mnakaribishwa.

5. Jumapili ijayo tarehe 11/08/2019 ni siku ya ubatizo na kurudi kundini.Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji

6. Leo tarehe 04/08/2019katika ibada zote ni siku yetu ya kukaribia madhabahuni kwa Mungu na sadaka ya upendo ya fungu la Kumi.itakayoambatana na maombi maalum kwa mwezi Agosti.Wenye mahitaji binafsi wayaandike na kuyawasilisha.

Neno: Zaburi 27:4, Wimbo: Kwaya Kuu (Sifa Zote)

7. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

Kwa mara ya Tatu tunatangaza ndoa za tarehe 10.08.2019

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Erick Lephy Gembe         na     Bi. Deykola Asimwe Rugaiganisa

 

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao matangazo.Karibu na duka letu la vitabu

8. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Wazo/Tegeta/Kunduchi/Bahari Beach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Nangawe
  • Mjini kati: Kwa Mama Aisa Oberlin
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Kowero
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Eng. na Bibi Zebadia Mushi
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Raphael Mollel
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Terry
  • Kinondoni: Kwa Prof G. Mmari

 

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.