MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 02 JULAI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI KIJANA MKRISTO NA MAISHA YA USHINDI

 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti:

3. Leo ni sikukuu ya Umoja wa Vijana hivyo ibada zote zitahudumiwa na Vijana.

4. Uongozi wa Kanisa Kuu Azania Front, pamoja na Kamati ya Misioni na Uinjilisti ya Baraza la Wazee, inatangaza kuwepo kwa mmiminiko wa Injili ya Yesu Kristo Katika wiki ya Injili ya Neno la Mungu  inayoanza jumapili ijayo tarehe 09 July hadi tarehe 16 July 2017. Huduma hii itafanyika ndani ya Kanisa hapa ushariani. Mnenaji atakuwa  Mwl Mgisa Mtebe. Kipindi cha Semina kitaanza saa 10.00 jioni. Karibuni wote katika semina hii kwani Mungu ana ujumbe wa wakati toka madhabahu yake ya Kanisa Kuu. Wote mnakaribishwa. Hakuna kiingilio. Aidha leo hakutakuwa na kipindi cha mafundisho, maombi na maombezi, ila kutakuwa na faragha ya maombi kuombea nguvu za Mungu juu ya madhabahu na Washarika kwa ujumla wao, na kujitayarisha kwa ajili ya semina ijayo. Wenye mzigo wa maombi hayo wanakaribishwa. Maombi yataanza saa 10.30 jioni hapa ndani kanisani. Hatutaombea wenye mahitaji bali tutaomba.

4. Jumamosi ijayo tarehe 08/07/2017 saa 3.00 asubuhi Usharika wa Mbezi Beach kutakuwa na ibada maalumu ambayo itajumuisha uchangiaji wa mfuko maalumu wa Elimu.  Ibada hii itaongozwa na Baba Askofu Alex G. Malasusa Wazee wakanisa wanaombwa kuhudhuria ibada hii bila kukosa na pia washarika wote mnakaribishwa sana kwenye ibada hiyo Muhimu.

5. Jumatano ijayo tarehe 05/07/2017 saa 11.00 jioni hapa Usharikani kutakuwa na kikao cha ibada za nyumba kwa nyumba. Mwenyekiti na Katibu wa kila Jumuiya wanaombwa kuhudhuria kikao hicho au wawakilishi wa jumuiya kama viongozi hawatakuwepo.

6. Jumapili ijayo tarehe 09/07/2017 kutakuwa na ubatizo wa watoto na kurudi kundini.  Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

Aidha siku hiyo tarehe 09/07/2017  katika ibada ya pili Saa 3.30 asubuhi Familia ya Mama Cecilia Joseph Korassa wa Upanga itamtolea Mungu Sadaka ya shukrani kwa ulinzi na mambo mengi mema aliyomtendea ikiwa pamoja na kumshukuru Mungu kwa kuwapa nguvu, kuwalinda tangu Mume wake Mpendwa Joseph Francis Korassa alipotwaliwa na Bwana tarehe 01/07/2012.

Neno: Wafilipo 1:21,Wimbo:Yesu ndiye Kiongozi wangu(TMW) 51.

 

7. Leo 02/07/2017 tutamtolea Mungu fungu la kumi.

 

8. NDOA

Ndoa za Washarika

Kwa mara ya Tatu tunatangaza ndoa za tarehe 08.07.2017

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Arnold Felician Itemba    na     Bi. Christine Mung’ong’o Hongera

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

9. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

Upanga: Kwa Bwana na Bibi Sabaya

Kinondoni: Kwa Prof na Bibi Saitiel Kulaba

Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Kowero

Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watatangaziana

Oysterbay/Masaki: Watatangaziana

Tabata: Watatangaziana

Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Sangiwa

Mjini kati: Watatangaziana

Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Watatangaziana

 

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza watashirikiana na Vijana.

 

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.