MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 26 NOVEMBA, 2017

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI UZIMA WA ULIMWENGU UJAO.

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Leo tarehe 26.11.2017 saa 10.00 jioni hapa Usharikani kutakuwa na faragha ya maombi ya Kamati ya Misioni na uinjilisti, wajumbe wote wa kamati wanaarifiwa ili wafike na tuanze kwa muda. Aidha wajumbe wa kamati nyingine za baraza wanakaribishwa katika maombi hayo ikiwa ni pamoja na wajumbe wa baraza la Wazee na msharika yeyote atayesukumwa kuungana na Kamati ya Misioni na Uinjilisti katika maombi hayo.  Njooni tumlilie Mungu juu ya Usharika wetu na familia zetu. Pia siku ya Alhamisi tarehe 30/11/2017 kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi. Kipindi hicho kitaongozwa na Mwinjilisti Emmanuel Franki toka KKKT Usharika wa Tumbi.  Wenye mahitaji wataombewa.

4. Ijumaa ya tarehe 15, Desemba 2017, Usharika umeandaa “Tamasha la Uimbaji la Krismas litakaloanza saa 11.30 jioni hadi saa 3:00 usiku. Tamasha litahusisha vikundi vyote vya kwaya hapa usharikani, Kwaya ya watoto wetu wa Shule ya Jumapili na kwaya ya ibada ya Kiingereza. Malengo ya tamasha hilo ni:-

Kuadhimisha Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo,

Vikundi vyote kwa pamoja KUMSHUKURU MUNGU kwa uongozi wake na ulinzi kwa Mwaka wote 2017, na kuomba uongozi wake kwa mwaka 2018.

 

5. Leo tutashiriki Chakula cha Bwana.  Washarika karibuni.

6. Washarika mnaombwa kujaza fomu kwa ajili ya utaratibu mpya wa namba za Bahasha. Wazee watagawa fomu hizo. Unapojaza fomu hii usisahau kujaza namba yako unayotumia sasa. Zoezi hili litaendelea hadi tarehe 10.12.2017.

7. Kwaya ya Tarumbeta Leo wanahudumu Usharika wa Bunju. Washarika tuwaombee.

8. Jumapili ijayo tarehe 03/12/2017  tutamtolea Mungu fungu la kumi.  Washarika tujiandae.

9. Ijumaa ijayo tarehe 01/12/2017 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha Baraza la Wazee. Wajumbe wote wanaombwa kuhudhuria kikao hiki muhimu.

10. Jumapili iyajo tarehe 03/12/2017 Kwaya ya Wanawake watakwenda kuhudumu Usharika wa Hananasifu.

11. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 02/12/2017

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Alpha Edward Mlenga              na     Bi. Tausi Abigail Fadhili Sade

 

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Philemon B. Mtinangi              na     Bi. Riziki A. Kidagho

 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

12. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Tom Njau
  • Kinondoni: Kwa Bibi Elinafika Mkubwa
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Itemba
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Prof. na Bibi W. Matuja
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Witson Moshi
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: kwa Bwana na Bibi Emannuel Matee
  • Mjini kati: Kwa Bibi Lydia Ngwale
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi David Korosso

 

Zamu: Zamu za wazee ni Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.