MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 23 JUNI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI TUNAITWA KUTENDA HAKI NA HURUMA

1.Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Wako wageni 2 waliotufikia na cheti

3. Tunamshukuru Mungu kwa jinsi anavyojidhihirisha tunapokutana kwa masomo, maombi na maombezi siku za alhamisi jioni.  Alhamisi ijayo tarehe 28/06/2018 kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi yatakayoanza saa 11.30 jioni. Wote mnakaribishwa.

4. Leo tutashiriki Chakula Cha Bwana.  Washarika karibuni.

5. Mkutano wa VICOBA ya Wajane na Wagane utafanyika jumamosi ijayo tarehe 30/06/2018 saa 3.00 asubuhi. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria. Aidha siku hiyo watafanya uchaguzi wa viongozi wao.

6. Uongozi wa Umoja wa vijana unapenda kuwatangazia vijana wote kuwa tarehe 01/07/2018 ni sikukuu ya Umoja wa vijana hivyo vijana wanaombwa kujiandikisha kwa nafasi mbalimbali kwa maandalizi ya siku hiyo. Wanaohitaji kujiandikisha baada ya ibada waonane na viongozi hapo nje.

7. Familia ya Bwana na Bibi Festo Sinkamba wamepata zawadi ya mtoto wa kike tarehe 22/06/2018 katika hospitali ya Dr. Hameer. Baba, Mama na Mtoto wanaendelea vizuri.

8. NDOA.

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 05/07/2018

SAA 08.00 MCHANA

  • Bw. Kiiza Emanzi Kemanzina Bi Joyce Dennis Kasyoba

TAREHE  07/07/2018

SAA 05.00 ASUBUHI

  • Bw. Emmanuel Tumsifu Jonas naBi Jacqueline Benezeth Benjamin

SAA 08.00 MCHANA

  • . Hans Ikamba Lasway             na     Bi. Ikumbo Charles  Nyange

SAA 10.00 JIONI

  • Bw. Christopher Michael Laban na Bi VeronicaJosephat Kweka

 

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 30/06/2018

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. John Ndisha Furahini               na     Bi Anneth Adolph Makenja

NDOA HII IFUATAYO ITAFUNGWA KANISA LA KATOLIKI PAROKIA YA UPANGA.

Bw. Derick Mujuni Kajukano           na     Bi. Anita Abednego Kinasha

 

Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

9. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

- Upanga: Kwa Mama Cecilia Korassa

- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki

- Mjini kati:  Kwa Eng. na Dr. Godfrey Moshi

- Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo

- Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Mchungaji Prudence Chuwa

- Tabata: Kwa Bwana na Bibi Oscar

                                               

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.