MATANGAZO YA USHARIKA

 TAREHE 25 JUNI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI WITO WA KUINGIA UFALME WA MUNGU.

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Wageni:  Wageni waliotufikia na cheti ni Daines Mdoe toka Mwanakwerekwe Zanzibar.
 1. Leo ndio siku ya mwisho ya wiki ya Injili ambayo tumekuwa na mfululizo wa mafundisho ibadani, Morning Glory na semina za ndani hapa Usharikani.  Semina ambayo neno linaloongoza ni Ufunuo 6:9 yenye kichwa kinachosema MAOMBI YANAYOWEZA KUKUNASUA KUTOKA KWENYE MADHABAHU ZILIZOSHIKILIA MAISHA YAKO inakamilika kwa semina leo mchana saa 9.30 jioni hapa usharikani. Imekuwa wiki yenye mafanikio makubwa sana kwani watu wamefundishwa neno, wameponywa na kufunguliwa.  Kwa wale ambao hawakuweza kufika leo nafasi ipo wanakaribishwa sana. Mnenaji ni Mtumishi Baraka Mbise wa KKKT Ubungo.
 1. Uongozi wa Umoja wa Vijana unawatangazia vijana wote na wazazi kuwa Tshirt za sikukuu ya vijana zinapatikana hapo nje chini ya mti, zipo za watoto na watu wazima pia.  Wazazi mnaombwa kuwanunulia vijana wetu na watoto wenu aidha vijana mnaombwa kuchukua fomu kwa ajili ya kongamano. Fomu zinapatikana hapo nje kwa viongozi wa vijana. Wazazi mnaombwa kuwahimiza vijana kushiriki kongamano hilo kwani ushiriki wa vijana Azania umekuwa hafifu sana katika makongamano yaliyopita.   
 1. Jumapili ijayo tarehe 02/07/2017 familia mbili zitamshukuru

Katika ibada ya kwanza, Familia ya Bwana na Bibi Abraham Salewi watamshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyowatendea.

Neno: Zaburi 9:1-2, Wimbo: TMW 51

Katika ibada ya pili, Lilian Elichilia Mboya atamshukuru Mungu kwa kutimiza miaka hamsini, anaomba washarika kumsindikiza.

Neno: Zab. 51:1-3, Wimbo: TMW 262

 1. Familia ya Bwana na Bibi Moses E. Mbise wamepata Baraka ya mtoto wa kiume tarehe 15/06/2017 katika hospitali ya Amana. Baba, Mama na Mtoto wanaendelea vizuri.
 1. Huduma ya MANA ikishirikiana na Kamati ya maandalizi ya Wamama wa Sayuni Dar es Salaam inawaalika wanawake wote kwenye Semina maalum ya Neno la Mungu kwa Wanawake itakayofanyika tarehe 01/07/2017 katika Kanisa la KKKT Mbezi Beach kuanzia saa 2 asubuhi – 9 alasiri. Wanawake wote mnakaribishwa sana.

 

 1. NDOA

Ndoa za Washarika

Kwa mara ya Pili tunatangaza ndoa za tarehe 08.07.2017

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Arnold Felician Itemba    na     Bi. Christine Mung’ong’o Hongera

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Upanga: Watatangaziana
 • Kinondoni: Bwana na Bibi Jackson Kaale
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Dk na Bibi David Ruhago
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Felix Mosha
 • Oysterbay/Masaki: Watatangaziana
 • Tabata: Watatangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Bwana na Bibi Sangiwa
 • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Stanley Mkocha
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Frank Korassa

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili.

 

ZAMU ZA WAZEE

IBADA I

Mzee Christine Shekidele       - Neno:  Zab. 61:1-8, Rum. 12:1-2, Mt. 9:9-13

Mzee Esther Mwaikambo       - Matangazo

Mzee Fred Msemwa               -  S/School

Mzee John Lyanga               -  Ndoa

                

IBADA II

Mzee Elibariki Moshi              - Neno:  Zab. 61:1-8, Rum. 12:1-2, Mt. 9:9-13

Mzee Harold Temu                - Matangazo

Mzee Lucy Mandara               - S/School

Mzee Ruth Mollel                   - Ndoa