MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 23 SEPTEMBA, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI UCHAGUZI WA BUSARA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3.Kamati ya Missioni na Uinjilisti inawaarifu washarika wote kuwa Wiki ijayo kuanzia Jumatatu tarehe 25/09/2017 hadi Jumapili tarehe 01/10/2017  kutakuwa na  semina ambayo  itahusu maombi.  Semina hiyo itaanza saa 11.00 jioni kila siku.  Mwalimu wa semina atakuwa Mchungaji Deogratius Msanya toka KKKT Moshi.  Vile vile atahudumu wiki nzima katika ibada za Morning Glory. Aidha, leo alasiri hatutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi bali tutaendelea na faragha ya maombi, agenda kuu ni kuuombea usharika wetu, washarika, na Semina itakayoanza kesho Jumatatu. Maombi yataanza saa 11.00 jioni, hapa usharikani. Wote mnakaribishwa.

4. Jumapili ijayo tarehe 01/10/2017 ni sikukuu ya Mikaeli na Watoto.

Washarika tuiombee siku hiyo.

5. Vitenge vya Miaka mia tano ya matengenezo ya Kanisa vipo.  Vitauzwa hapo nje na viongozi wa Umoja wa Wanawake kwa bei ya sh. 15,000/=.  Aidha Vitenge vya Kiharaka navyo bado vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya shilingi elf 10.  Washarika karibuni.

6. Jumamosi ijayo tarehe 30/09/0217 saa 3.00 asubuhi Kutakuwa na Mkutano wa VICOBA vya Wajane na Wagane wa Azania Front. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria mkutano huo.

7. Jumapili ijayo tarehe 01/10/2017 familia mbili zitamtoea Mungu shukrani.

Familia ya Bwana na Bibi Buchanagandi itatoa sadaka ya shukrani  kwa kurudi salama kutoka kwenye matibabu, kuhamia nyumba mpya, kufikisha miaka 38 ya ndoa yao na mambo mengi aliyowatendea. Shukrani hii itafanyika ibada ya Kwanza saa 1.00 asubuhi.

Neno: Zaburi 103:1-5, 11-13. Wimbo: Kwaya ya Upendo(Uhai nilionao)

Familia ya Advocate Victoria Mandari nao watatoa shukrani ya pekee kwa mambo mema Mengi Mungu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na watoto wake wote kumaliza masomo salama nje ya nchi, mtoto wake Samuel Mpangile kufaulu vizuri Shahada yake ya Finance na kupata First Class pamoja na kupata kazi Uingereza. Shukrani hii itafanyika ibada ya pili saa 3.30 asubuhi.

Neno: Zaburi 9: 1-2, Zaburi 95:2-3,  Wimbo 405.

 

8. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 30/09/2017

NDOA HII ITAFUNGWA  KANISA LA ANGLIKAN NEEMA CATHEDRAL RUBUNGO

Bw. Jossam Mugisha Mabaraza       na    Bi. Magreth Ernest Mtui

 

KWA MARA YA TATU NDOA  YA  TAREHE 01/10/2017

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Victor Eliazer Mwasele      na    Bi. Anastazia Nicolaus Kampa

 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

9. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: kwa Mama Cecilia Korassa
  • Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaula
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Itemba
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Mzee Arnold Kilewo
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi David Mollel
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: kwa Mama Korroso
  • Mjini kati: Kwa Bibi Omega Mongi
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:Kwa Bwana na Bibi Lawlence Mlaki

Zamu: Wazee wote  watakuwa Zamu.

 

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.