MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 23 JULAI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI AMRI YA UPENDO

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti:
 1. Leo tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika Karibuni.
 1. Uongozi wa Kanisa Kuu Azania Front, pamoja na Kamati ya Misioni na Uinjilisti ya Baraza la Wazee, inatangaza kuwepo kwa mmiminiko wa Injili ya Yesu kristo katika wiki ya Injili ya Neno la Mungu inayoanza Jumapili ijayo tarehe 30 Julai saa 9.30 alasiri hadi tarehe 06 Agosti 2017.  Huduma hii itafanyika ndani ya Kanisa hapa Usharikani. Mnenaji atakuwa Mwinjilisti Grace Kisuu.  Karibuni wote katika semina hii kwani Mungu ana ujumbe wa wakati toka madhabahu yake ya Kanisa Kuu. Wote mnakaribishwa.  Hakuna kiingilio. Aidha leo hakutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi, tutaanza tena Alhamisi tarehe 27/07/2017 saa 11.30 jioni.
 1. Jumamosi ijayo tarehe 29/07/2017 saa 3.00 asubuhi hapa usharikani kutakuwa na kikao cha wajane na Wagane. Wajumbe  wote mnaombwa kuhudhuria siku hiyo.
 1. Umoja wa Vijana unapenda kuwakumbusha  Vijana kuwa leo tarehe 23/07/2017 kutakuwa na sikukuu ya vijana Kijimbo itafanyika usharika wa Segerea kuanzia saa 7.00 mchana. Vijana wote wanatakiwa kushiriki tukio hilo. Vazi ni Tshirt zilizovaliwa  sikukuu vijana hapa usharikani.
 1. Leo mara baada ya ibada ya pili kutakuwa na kikao cha Umoja wa Wanaume Azania Front  kwa ajili ya kupitia rasimu ya muongozo wa Umoja huo.  Hivyo wanaume wote mnaombwa kubaki ndani mara baada ya ibada hiyo ya pili.
 1. Tunapenda kuwakumbusha washarika wanaodaiwa madeni ya mavuno ya Mwaka jana 2016 na miaka ya nyuma warejeshe madeni yao ofisi ya wahasibu.
 1. Jumamosi ijayo tarehe 29.07.2017 ndiyo siku ya maonesho ya watoto walemavu yatakayofanyika kituo cha Diakonia Mtoni. Katika maonesho hayo kutaoneshwa na kuuzwa kazi za mikono zilizofanywa na watoto hao. Washarika mnaombwa na kukumbushwa kuhudhuria maonesho hayo, na wale walioahidi kutoa michango na kupokea kadi zilizotayarishwa na watoto hao wanakumbushwa kuwasilisha michango yao kwa mhasibu kabla ya siku hiyo na kuhudhuria kama walivyoalikwa kwenye kadi walizochukua.
 1. Ijumaa ijayo tarehe 28/07/2017 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha Baraza la Wazee.  Wazee wote wanatakiwa kuhudhuria. Aidha kamati za Baraza zinatakiwa kutayarisha ripoti za kamati zao kwa ajili ya kikao hicho.
 1. Jumapili ijayo tarehe 30/07/2017 familia mbili zitamtolea Mungu shukrani:-
 •  Familia ya Bwana na Bibi Allen Kaduri watamshukuru Mungu kwa Bwana Allen Kaduri kutimiza miaka 80 pamoja na kutimiza miaka 50 ya ndoa yao.

Neno: Zaburi 103:1-5, Maombolezo 3:22-24

Wimbo: (Zawadi gani) toka Kwaya ya vijana, na (Maharusi

               Wanapendeza) -  toka Kwaya Kuu

 

 •  Familia ya Bwana Festo na Bibi Josephine Mtumbe watamshukuru Mungu kwa kuwawezesha kufunga ndoa yao salama na mambo mengi mema aliyowatendea.

Neno:  Zaburi 138:1-2

Wimbo: (Sita Choka) toka Kwaya ya Vijana

 

 1. NDOA

Hakuna ndoa za Washarika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

 

 • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mduma
 • Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaula
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi  James Monyo
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Mama Erica Byabato
 • Oysterbay/Masaki: Kwa Bwana na Bibi Elibariki Moshi
 • Tabata: Watatangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi S. Jengo
 • Mjini kati: Kwa Mama Hilda Rwansane
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:Kwa Bwana na Bibi Mlagha

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.  

 

Z