MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 21 JANUARI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI TUKUE KATIKA UMOJA – SIKU YA CCT

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti. Na kama kuna wageni walioshiriki nasi mara ya kwanza wasimame ili tuweze kuwakaribisha.

3. Leo hatutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi hapa usharikani, kipindi hiki kitafanyika  Alhamisi ijayo tarehe 25-1-2018 saa 11:30 jioni

4. Familia ya Marehemu Mama Mpendwa Winnie Kuzilwa wanapenda kutoa shukrani kwa mambo mengi mema Mungu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kuwatia nguvu tangu mama Winnie aliyetwaliwa na Bwana miaka 19 iliyopita.

Neno: Zaburi 100:1-5, Wimbo: TMW 405

5. Wazazi/Walezi wenye watoto walio na umri wa kuanza kipaimara walete majina ya watoto katika ofisi za Usharika, kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Aidha darasa la mwaka wa Kwanza litafunguliwa  Jumamosi tarehe 27-01-2018 saa 7.00 Mchana.

6. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwajulisha Wanawake kuwa Jumapili ijayo tarehe 28/01/2018 watamshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na kumaliza mwaka salama na kuingia mwaka mpya. Aidha kama ilivyo kawaida kila mwaka mwezi wa tatu wanawake wanakuwa na matukio mengi  pamoja na maombi ya dunia na kuongoza ibada. Hivyo  siku ya jumamosi tarehe 27/01/2018 saa 3.00 asubuhi wanawake wanaombwa kufika  kwa ajili ya maandalizi ya matukio hayo yakwamba Kila mwanamke aseme atafanya nini.

7. Jumanne ijayo tarehe 23/01/2018 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha Kamati ya utendaji ya Baraza la Wazee.  Kamati zote zikutane kwa ajili ya ripoti ya Kikao hicho. Aidha Ijumaa tarehe 26/01/2018 saa 11.00 jioni kutakuwa na maombi ya Baraza ya Wazee.

8. Jumapili ijayo tarehe 28/01/2017 tutashiriki chakula cha Bwana.  Kama ilivyo kawaida siku ya Chakula cha Bwana ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi. Washarika tukiandae

9. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 10/02/2018

Bwana Gustav Bapas Mphusu                 na     Rose Juma Tang’are

Matangazo mengine ya Ndoa 0yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

10. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

- Upanga: Kwa Tom Njau

- Kinondoni: Kwa Prof na Bibi Saitiel Kulaba

- Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi Kowero

- Oysterbay/Masaki: Kwa Capt na Bibi J. MKony

- Mjini kati:  Kwa Bwana na Bibi G. Mnyitafu

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.