MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 20 AGOSTI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU KWA WATU WOTE.

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti:

3. Leo hatutakuwa na kipindi cha Maombi na Maombezi hapa Usharikani, ila huduma itaendelea siku ya Alhamisi 24/08/2017 Kipindi kitaongozwa na Mwinjilisti Emmanuel Frank wa KKKT Tumbi.Wote mnakaribishwa.

4. Vitenge vya Kiharaka bado vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya shilingi elf 10.Kama umeshanunua unaweza kumnunulia ndugu, rafiki ili tuweze  kufanikisha ujenzi wa kituo chetu cha Kiroho Kiharaka.

5. Jumanne ijayo tarehe 22/08/2017 saa 11.00 jioni. Kutakuwa na kikao kifupi cha Baraza la Wazee. Wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria.

6. Kwaya yetu ya Tarumbeta leo inahudumu Mtaa wa Misugusugu kwa ajili ya tendo la Kufungua Nyumba ya ibada ya Mtaa huo.

7. Jumapili ijayo tarehe 27/08/2017 tutashiriki Chakula cha Bwana.Hivyo ibada ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi. Washarika tujiandae.

8. Usharika kupitia Kamati ya Uhusiano na Habari, una mkakati wa kuwahabarisha Washarika kwa kijarida kitakachokua na habari mbali mbali za Usharika, vikundi na mitaa yake.Kijarida hicho kitatoka kila baada ya miezi 3.Kamati inatafuta mtu mwenye taaluma husika kufanya kazi hiyo, kwa ujira na maelewano maalum.Kwa mawasiliano zaidi muone Mzee T. Mlaki, Mzee C. Swai au katibu wa Usharika.

9. Jumapili tarehe 27.08.2017 familia mbili zitamtolea Mungu Shukrani.

10. Familia ya Mchungaji na Mama Astoni Kibona watamshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 40 ya ndoa yao ikiwa ni pamoja na mambo mengi mema aliyowatendea. Tendo hili litafanyika katika ibada ya pili.

Neno: Zaburi 116:12-14, Wimbo Kwaya Kuu (Nitayainua macho yangu) na TMW 263

11. Joyce Kasyanju Mgaza naye atamshukuru Mungu kwa kumshika na kuendelea kumtunza kipindi chote kigumu tangu Mume wake Mpendwa Bernard V. Mgaza alipotwaliwa na bwana tarehe 26/08/2015.

Neno Zaburi, 11:1-2 na Zaburi 23, Wimbo: TMW 295(Mungu amenihurumia).

 

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 09/09/2017

SAA 08.00 MCHANA

Bw. Samson Felix mkwama             na     Bi. Naomi Joel Kiangi

 

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 26/08/2017

SAA 10.00 JIONI

Bw. Winston Churchil katwaza        na     Bi. Lucy Zebedayo Lushiku

 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Rabiel Kimaro
  • Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Jackson Kaale
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Theophilus Mlaki
  • Tabata: Watatangaziana
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi C. Lyimo
  • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi G. Mnyitafu

 

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili

 

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.