KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA

DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA

LEO TAREHE 16 OKTOBA, 2016

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI TUKAZE MWENDO KATIKA KRISTO

 

  1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
  1. Wageni: Hakuna Wageni waliotufikia na Cheti Kama kuna wageni wengine walioshiriki nasi wasimame ili tuwakaribishe.
  1. Leo jumapili kutakuwa na kipindi cha maombi ya kufunguliwa waliofungwa katika uchumi, biashara na ustawi binafsi.  Pia kutakuwa na maombi kwa ajili ya Wagojwa. Mnenaji atakuwa Mtumishi Sweetbert Lugemalila ambaye atakuwepo kanisani kuanzia saa 9.00  kwa ajili ya mahitaji binafsi.  Alhamisi ijayo pia kutakuwa na maombi na maombezi kuanzia saa 11.00 jioni.  Wagonjwa na wenye shida mbalimbali pia watapata huduma siku hiyo.  Wote mnakaribishwa na muwaarifu wengine.

 

  1. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwashukuru wazazi kwa kuwaruhusu  wanafunzi wa Kipaimara kwa ajili mafundisho ya afya yaliyofanyika jana jumamosi tarehe 15/10/2016 hapa Usharikani. Mungu awabariki sana
  1. Jumamosi tarehe 22.10.2016 saa 3.00 asubuhi kutakuwa na kikao cha Wajane. Wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria
  1. Jumapili ijayo tarehe 23/10/2016 itakuwa ni sikukuu ya mavuno, hivyo ibada itakuwa ni moja itakayoanza saa 2.00 asubuhi. Washarika tuiombee siku hiyo. Aidha leo wazee watagawa bahasha kwa ajili ya mavuno hayo.
  1. Familia ya Bwana na Bibi Victor Bernard Machange wamepata zawadi ya mtoto wa kike tarehe 10.10.2016 katika hospitali ya Taifa Muhimbili. Baba, Mama na Mtoto wana afya njema.
  1. NDOA:

NDOA ZA WASHARIKA

Kwa mara ya tatu tunatangaza ndoa za tarehe 23.11.2016

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Benet Muta Kibira              na     Bi. Janeth David Makangila

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu

  1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

 

  • Upanga:  Kwa Rabiel Kimaro
  • Kinondoni: Kwa Mama T. Nziku
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watatangaziana
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Mama Chipeta
  • Tabata: Watatangaziana
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Mzee Kuzilwa
  • Mjini kati: Watatangaziana
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:  Kwa Bwana na Bibi Nangawe

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki