MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 14 JANUARI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI MUNGU HUBARIKI NYUMBA ZETU

 1. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
 2. Leo hatutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi hapa usharikani, kipindi hiki kitafanyikaAlhamisi ijayo tarehe 18-1-2018 saa 11:30 jioni
 3. Leo katika ibada zote mbili tutakuwa na maombi ya kumshukuru kwa Mungu, pamoja na kumtolea Mungu shukrani kwa kutuvusha mwaka, pia kujikabidhi kwa Mungu katika mwaka huu mpya wa 2018 tulete mahitaji yetu kwa Mungu aliye na majibu ya maisha yetu.
 4. Tarehe 27-01-2018 siku ya Jumamosi, kutakuwa na mkutao wa VICOBA ya wajane na wagane wa Azania front. Muda ni saa tatu asubuhi wahusika wote mnaombwa kuhudhuria.
 5. Tunapenda kuwataarifu Washarika wote kuwa namba mpya za Bahasha tayari zimebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu na Mlango mkubwa nyuma kuingia kwenye Bahasha. Namba hizi mpya zinaanza kutumikakuanzia Januari 2018.Mungu awabariki kwa utayari wenu.

6. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia washarika wote kuwa Jumapili ijayo tarehe 21/01/2018 katika ibada ya pili kutakuwa  na tendo la kuzindua Kinanda chetu kipya (PIPE ORGAN). Tendo hili litafanywa na Askofu Alex Gehazi Malasusa.

7. Wazazi/Walezi wenye watoto walio na umri wa kuanza kipaimara walete majina ya watoto katika ofisi za Usharika, kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Aidha darasa la mwaka wa pili limefunguliwa jana Jumamosi tarehe 13-01-2018

8. Tarehe 21/01/2018 katika ibada ya pili familia ya Chaplain na Mama Charles Mzinga watamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyowatendea ikiwa ni pamoja na Kumponya kabisa Mch. Charles Mzinga aliyekuwa anapata matibabu nchini India.

9. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwajulisha kuwa shule zimefunguliwa na watoto wetu wa Donbosco wameanza shule. Kama ilivyo kawaida yetu tunaomba michango yenu ya hali na mali ili tuweze kuwalipia Ada. Fedha zipelekwe kwa Mhasibu wa usharika au viongozi wa Umoja wa Wanawake. Mungu awabariki. Aidha Jumamosi ijayo tarehe 20/01/2018 Uongozi wa Wanawake Jimbo la Kati umeandaa maombi ya kumshukuru Mungu.maombi hayo yatafanyika Mtaa wa Chanika kuanzia saa 3.00 asubuhi.Wanawake wote mnaombwa kuhudhuria.

10. Jumanne ijayo tarehe 23/01/2018 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha Kamati ya utendaji ya Baraza la Wazee.Kamati zote zikutane kwa ajili ya ripoti ya Kikao hicho. Aidha Ijumaa tarehe 26/01/2018 saa 11.00 jioni kutakuwa na maombi ya Baraza ya Wazee.

 

11. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 20/01/2018

SAA 8.00 MCHANA

Bwana Noel Gadiel Mushi               na     Mary Edward Mashelle

SAA 9:00 ALASIRI

Bwana David James Kaunda                   na     Joyce N. Luvanda

 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

12. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

 • Upanga: Kwa ………….
 • Kinondoni: ………….
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: ………….
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Mchungaji Charles Mzinga
 • Oysterbay/Masaki: ………….
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Simon Jengo
 • Mjini kati:  Kwa Bwana na Bibi George Mnyitafu
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:…………..
 • Tabata:  …………………….

 

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.