MATANGAZO YA USHARIKA

  TAREHE 09 JULAI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI TUNAITWA KUTENDA HAKI NA HURUMA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na cheti:

3. Tarehe 22/07/2017 saa 3.00 asubuhi hapa usharikani kutakuwa na kikao cha wajane na Wagane. Wajumbewote mnaombwa kuhudhuria siku hiyo.

4. Uongozi wa Kanisa Kuu Azania Front, pamoja na Kamati ya Misioni na Uinjilisti ya Baraza la Wazee, inatangaza kuwepo kwa mmiminiko wa Injili ya Yesu Kristo Katika wiki ya Injili ya Neno la Mungu inayoanza leo jumapili tarehe 09 July hadi tarehe 16 July 2017. Huduma hii itafanyika ndani ya Kanisa hapa ushariani. Mnenaji atakuwaMwl Mgisa Mtebe. Kipindi hiki cha Semina leo kitaanza saa 10.00 jioni. Wote mnakaribishwa. Hakuna kiingilio.

5. Jumatatu ijayo Tarehe 10.07.2017 yaani kesho mpaka 14.07.2017 Dayosisi kwa kushirikiana na Madaktari wa meno toka Marekani watatoa bure huduma ya Kutibu na kusafishameno katika Zahanati ya Mtoni Temeke. Wote wanakaribishwa muda ni saa 2.00 asubuhi mpaka saa 9.00 alasiri.

6. NDOA

Hakuna ndoa za Washarika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

7.  Ibada za Nyumba kwa Nyumba

Upanga: Kwa Bwana na Bibi Cuthbert Swai

Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Edward Mkonyi

Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watatangaziana

Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Kaduri

Oysterbay/Masaki: Watatangaziana

Tabata: Watatangaziana

Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Watatangaziana

Mjini kati: Kwa Mama Omega Mongi

Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Simbeye

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.