Date: 
16-09-2020
Reading: 
MARKO 12:41-44

WEDNESDAY 16TH SEPTEMBER 2020 MORNING                                      

Mark 12:41-44 New International Version (NIV)

41 Jesus sat down opposite the place where the offerings were put and watched the crowd putting their money into the temple treasury. Many rich people threw in large amounts. 42 But a poor widow came and put in two very small copper coins, worth only a few cents.

43 Calling his disciples to him, Jesus said, “Truly I tell you, this poor widow has put more into the treasury than all the others. 44 They all gave out of their wealth; but she, out of her poverty, put in everything—all she had to live on.”

It is not how much we give that matters, but how we give. The widow gave more because she gave sacrificially. We can give sacrificially in many ways: our time, our homes in terms of hospitality, sharing other things we own, and our lives – serving God.


JUMATANO TAREHE 16 SEPTEMBA 2020 ASUBUHI                               

MARKO 12:41-44

41 Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi.
42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa.
43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;
44 maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia.

Haijalishi ni kiasi gani tunamtolea Mungu, bali ni kwa namna gani tunamtolea. Mama mjane alitoa zaidi kwa sababu alitoa vyote alivyokuwa navyo. Tunaweza kujitoa kwa njia nyingi: muda wetu, nyumba zetu kwa kuonyesha ukarimu, kutoa mali zetu kwa ajili ya wahitaji, na maisha yetu katika kumtumikia Mungu.