Date: 
27-04-2017
Reading: 
Mark 6:1-6 (NIV)

THURSDAY 27TH APRIL 2017 MORNING                                

Mark 6:1-6  New International Version (NIV)

A Prophet Without Honor

1 Jesus left there and went to his hometown, accompanied by his disciples. When the Sabbath came, he began to teach in the synagogue, and many who heard him were amazed.

“Where did this man get these things?” they asked. “What’s this wisdom that has been given him? What are these remarkable miracles he is performing? Isn’t this the carpenter? Isn’t this Mary’s son and the brother of James, Joseph,[a] Judas and Simon? Aren’t his sisters here with us?” And they took offense at him.

Jesus said to them, “A prophet is not without honor except in his own town, among his relatives and in his own home.” He could not do any miracles there, except lay his hands on a few sick people and heal them.He was amazed at their lack of faith.

Jesus Sends Out the Twelve

Then Jesus went around teaching from village to village.

Footnotes:

  1. Mark 6:3 Greek Joses, a variant of Joseph

In Nazareth where Jesus grew up people did not really understand who He is. They thought that He was just a carpenter and son of Joseph and Mary. People did not believe or understand that He is the Son of God.

Do we really understand who Jesus is?  Have you just heard about Jesus or do you know him personally as your Lord and Saviour?  

ALHAMISI TAREHE 27 APRILI 2017 ASUBUHI                               

MARKO 6:1-6

1 Akatoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao; wanafunzi wake wakamfuata. 
2 Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? 
3 Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. 
4 Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. 
5 Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. 
6 Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazunguka-zunguka katika vile vijiji, akifundisha. 
 

Kule Nazareti, mji ambao Yesu alikulia, watu wengi hawakumwelewa. Majirani zake wengi walimwona kama mtu wa kawaida, fundi seremala, na mwana wa Yusufu na Maria. Hawakuelewa kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu na Mwokozi wa Ulimwengu.

Wewe Je! Unamwelewa Yesu vizuri? Ni nani kwako? Umemsikia au unamfahamu kama Bwana na Mwokozi wako?