Date: 
27-10-2017
Reading: 
LUKE 8:49-56 NIV (LUKA 8:49-56)

FRIDAY 27TH OCTOBER MORNING

LUKE 8:49-56 New International Version

Jesus Raises a Dead Girl

49 While Jesus was still speaking, someone came from the house of Jairus, the synagogue leader. “Your daughter is dead,” he said. “Don’t bother the teacher anymore.”

50 Hearing this, Jesus said to Jairus, “Don’t be afraid; just believe, and she will be healed.”

51 When he arrived at the house of Jairus, he did not let anyone go in with him except Peter, John and James, and the child’s father and mother. 52 Meanwhile, all the people were wailing and mourning for her. “Stop wailing,” Jesus said. “She is not dead but asleep.”

53 They laughed at him, knowing that she was dead. 54 But he took her by the hand and said, “My child, get up!” 55 Her spirit returned, and at once she stood up. Then Jesus told them to give her something to eat. 56 Her parents were astonished, but he ordered them not to tell anyone what had happened.

There is no problem that is too big for Jesus. All we need to do is have faith in him, and take our troubles to Him and believe that he will take care of them. What is troubling you in your life? Cast all your anxiety on him because he cares for you. (1Peter 5:7)

IJUMAA TAREHE 27/10/2017 ASUBUHI

LUKA 8:49-56

YESU AMFUFUA MSICHANA

49 Alipokuwa akinena hayo, alikuja mtu kutoka nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha kufa; usimsumbue mwalimu.
50 Lakini Yesu aliposikia hayo, alimjibu, Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa.
51 Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye.
52 Na watu wote walikuwa wakilia na kumwombolezea; akasema, Msilie, hakufa huyu, bali amelala usingizi tu.
53 Wakamcheka sana, maana walijua ya kuwa amekwisha kufa.
54 Akamshika mkono, akapaza sauti, akisema Kijana, inuka.
55 Roho yake ikamrejea, naye mara hiyo akasimama. Akaamuru apewe chakula.
56 Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini akawakataza wasimwambie mtu lililotukia.

Hakuna jambo linalomshida Yesu, tunahitaji kuwa na Imani na kumpelekea shida zetu na kuamini atatenda. Je una jambo gani linalokusumbua? Peleka mzigo wako kwa Yesu, naye atakupumzisha. (Soma 1 Petro 5:7)