Date: 
04-07-2018
Reading: 
Luke 2:41-52 (Luka 2:41-52)

WEDNESDAY 4TH JULY 2018 MORNING                          

Luke 2:41-52 New International Version (NIV)

The Boy Jesus at the Temple

41 Every year Jesus’ parents went to Jerusalem for the Festival of the Passover. 42 When he was twelve years old, they went up to the festival, according to the custom. 43 After the festival was over, while his parents were returning home, the boy Jesus stayed behind in Jerusalem, but they were unaware of it. 44 Thinking he was in their company, they traveled on for a day. Then they began looking for him among their relatives and friends. 45 When they did not find him, they went back to Jerusalem to look for him. 46 After three days they found him in the temple courts, sitting among the teachers, listening to them and asking them questions. 47 Everyone who heard him was amazed at his understanding and his answers. 48 When his parents saw him, they were astonished. His mother said to him, “Son, why have you treated us like this? Your father and I have been anxiously searching for you.”

49 “Why were you searching for me?” he asked. “Didn’t you know I had to be in my Father’s house?”[a] 50 But they did not understand what he was saying to them.

51 Then he went down to Nazareth with them and was obedient to them. But his mother treasured all these things in her heart. 52 And Jesus grew in wisdom and stature, and in favor with God and man.

Footnotes:

  • Luke 2:49 Or be about my Father’s business

This week we are thinking about youths and their testimony.

In the passage above we hear of an incident which took place when Jesus was only 12 years old. He was the age of one of our Confirmation class students.

We pray for young people who are preparing for Confirmation that they may truly seek God and grow in faith and desire to follow Jesus all their lives.  

JUMATANO TAREHE 4 JULAI 2018 ASUBUHI                                              

LUKA 2:41-52

41 Basi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. 
42 Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu; 
43 na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari. 
44 Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao; 
45 na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. 
46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 
47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. 
48 Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. 
49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? 
50 Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia. 
51 Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake. 
52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.

Wiki hili tunatafakari kuhusu vijana na ushuhuda wao.

Somo hapa juu inamhusu Yesu Kristo wakati alikuwa kijana wa miaka 12 tu. Alitafuta kujifunza zaidi kuhusu Mungu.

Alikuwa umri sawa na Mwanafunzi wa Kipaimara. Tuwaombee wanafunzi wa Kipaimara wamtafute Mungu na kujifunza kwa bidii na kutamani kumfuata Yesu Kristo maisha yao yote.