Date: 
27-11-2019
Reading: 
Luke 12:35-43

WEDNESDAY 27TH NOVEMBER 2019  MORNING    

Luke 12:35-43 New International Version (NIV)

Watchfulness

35 “Be dressed ready for service and keep your lamps burning, 36 like servants waiting for their master to return from a wedding banquet, so that when he comes and knocks they can immediately open the door for him. 37 It will be good for those servants whose master finds them watching when he comes. Truly I tell you, he will dress himself to serve, will have them recline at the table and will come and wait on them. 38 It will be good for those servants whose master finds them ready, even if he comes in the middle of the night or toward daybreak. 39 But understand this: If the owner of the house had known at what hour the thief was coming, he would not have let his house be broken into. 40 You also must be ready, because the Son of Man will come at an hour when you do not expect him.”

41 Peter asked, “Lord, are you telling this parable to us, or to everyone?”

42 The Lord answered, “Who then is the faithful and wise manager, whom the master puts in charge of his servants to give them their food allowance at the proper time? 43 It will be good for that servant whom the master finds doing so when he returns. 

To have a lamp on would be an indicator that you were prepared even at night. It also meant you were still up and available. It also showed the ability to receive visitors. If you went out at night, you would bring a lamp to light your way so that you could avoid stumbling around in the dark. It would also enable others to see you, which would be very important when you are trying to meet with others at night. 

Let us pray that today we can all say that we love our Lord and we are waiting and watching.  Not only that, but we also must be serving.


ALHAMISI TAREHE 27 NOVEMBA 2019   ASUBUHI  LUKA 12:35-43

Kukesha 

35 Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka;
36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
38 Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.
39 Lakini fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi, angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa.
40 Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.
41 Petro akamwambia, Bwana, mithali hiyo umetuambia sisi tu, au watu wote pia?
42 Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?
43 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo.

Kuwa na taa inayowaka ilikuwa ni ishara ya kuwa macho na utayari; na kuwa na uwezo wa kuwakaribisha wageni. Ikiwa ulitoka nje usiku, ungechukua taa ili usije kujikwaa gizani. Ingeliwasaidia pia wengine kukuona, ambapo ni jambo muhimu sana hasa pale unapotaka kukutana na watu wakati wa usiku. 

Tumwombe Mungu kuwa  leo sote tunaweza kusema tunampenda na kwamba tunakesha na kungojea kurudi kwake. Siyo hivyo tu, bali ni lazima tuwe tunamtumikia.