Date: 
02-03-2021
Reading: 
Luka 20:9-16

Jumanne Tarehe 02.03.2021, asubuhi

Ukatili ni uovu

Luka 20:9-16

Akaanza kuwaambia watu mfano huu; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akapangisha wakulima, akaenda akakaa katika nchi nyingine muda mrefu.
10 Na wakati wa mavuno alituma mtumwa kwa wale wakulima ili wampe baadhi ya matunda ya mizabibu; wakulima wakampiga wakamfukuza mikono mitupu.
11 Akatuma na mtumwa mwingine. Wakampiga huyu naye, wakamwaibisha wakamfukuza mikono mitupu.
12 Akamtuma na wa tatu; huyu naye wakamtia jeraha, wakamtupa nje.
13 Basi, bwana wa shamba la mizabibu alisema, Nifanyeje? Nitamtuma mwanangu, mpendwa wangu; yamkini watamheshimu yeye.
14 Lakini, wale wakulima walipomwona, walishauriana wao kwa wao, wakisema, Huyu ndiye mrithi; haya, na tumwue, ili urithi uwe wetu.
15 Wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua. Basi, bwana wa shamba la mizabibu atawatendeje?
16 Atakuja na kuwaangamiza wakulima wale, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine. Waliposikia hayo walisema, Hasha! Yasitukie haya!

Yesu Kristo ndiye mrithi halali na mmiliki wa shamba la mzabibu; na jambo muhimu kwa watumishi wake ni kumzalia matunda. Yesu alitaka kuwatia moyo wale watumishi waaminifu ambao wanapigwa na kutupwa nje ya shamba la mzabibu kuzidi kuwa waaminifu. Hivyo, tunapaswa kujitoa na kumtumikia ili tusipatwe na ile hukumu.


Tuesday 2nd March 2021

Luke 20:9-16

The Parable of the Tenants

He went on to tell the people this parable: “A man planted a vineyard, rented it to some farmers and went away for a long time. 10 At harvest time he sent a servant to the tenants so they would give him some of the fruit of the vineyard. But the tenants beat him and sent him away empty-handed. 11 He sent another servant, but that one also they beat and treated shamefully and sent away empty-handed. 12 He sent still a third, and they wounded him and threw him out.

13 “Then the owner of the vineyard said, ‘What shall I do? I will send my son, whom I love; perhaps they will respect him.’

14 “But when the tenants saw him, they talked the matter over. ‘This is the heir,’ they said. ‘Let’s kill him, and the inheritance will be ours.’ 15 So they threw him out of the vineyard and killed him.

“What then will the owner of the vineyard do to them? 16 He will come and kill those tenants and give the vineyard to others.”

When the people heard this, they said, “God forbid!”

Read full chapter

Jesus Christ is the rightful heir and owner of the vineyard; and the main thing is for His servants to bear fruit for Him. He wanted to encourage His faithful servants who get beat up and thrown out of the vineyard to keep on being faithful. Therefore, we both submit and serve Him, or we will face His certain judgment.