Date: 
14-12-2021
Reading: 
Luka 1:46-53

Hii ni Advent 

Jumanne asubuhi tarehe14.12.2021

Luka 1:46-53

46 Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;

48 Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;

49 Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu.

50 Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.

51 Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;

52 Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge amewakweza.

53 Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.

Itengenezeni njia ya Bwana 

Mariamu baada ya kupokea ujumbe toka Bwana uliohusu kumzaa Yesu, anafanya sala, moyo wake ukimwadhimisha Bwana kama Mungu mwenye enzi, mfalme wa vyote mbinguni na duniani.

Katika utume tulionao, ni muhimu kuendelea kutumika kwa uaminifu, tukimpa Yesu nafasi mioyoni mwetu. Tuepuke njia zisizofaa, mioyo yetu ikimwadhimisha Bwana kwa utukufu wake.

Siku njema.