Date: 
30-04-2022
Reading: 
Luka 13:33-36

Jumamosi asubuhi tarehe 30.04.2022

Luka 11:33-36

33 Hakuna mtu awashaye taa na kuiweka mahali palipositirika, au chini ya pishi; bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuuona mwanga.

34 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote unao mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao una giza.

35 Angalia basi, mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza.

36 Basi kama mwanga umeenea katika mwili wako wote, wala hauna sehemu iliyo na giza, mwili wako wote utakuwa na mwanga mtupu; kama vile taa ikumulikiapo kwa mwanga wake.

Yesu Kristo ajifunua kwetu;

Yesu anafundisha kwa mfano wa mwanga, kwamba taa ikiwashwa lazima iwekwe mahali pa wazi ili iangaze. Yesu anasema taa ya mwili ni jicho, hivyo ni muhimu jicho kuwa safi, ili mwili wote upate mwanga. Yesu anasisitiza waaminio kuangalia mwanga ulioko ndani yao usiwe giza.

Matendo yetu na maneno yanatakiwa kuangaza watu wote, na kwa njia hiyo Yesu atukuzwe, watu wake wakiokolewa. Mwanga ukiwa kwetu hatutaona giza, yaani Yesu akiwa upande wetu tunashinda dhambi.

Ubarikiwe.