Date: 
20-03-2018
Reading: 
Leviticus 16:20-28 (Walawi 16:20-28)

TUESDAY 20TH MARCH 2018 MORNING                                 

Leviticus 16:20-28 New International Version (NIV)

20 “When Aaron has finished making atonement for the Most Holy Place, the tent of meeting and the altar, he shall bring forward the live goat.21 He is to lay both hands on the head of the live goat and confess over it all the wickedness and rebellion of the Israelites—all their sins—and put them on the goat’s head. He shall send the goat away into the wilderness in the care of someone appointed for the task. 22 The goat will carry on itself all their sins to a remote place; and the man shall release it in the wilderness.

23 “Then Aaron is to go into the tent of meeting and take off the linen garments he put on before he entered the Most Holy Place, and he is to leave them there. 24 He shall bathe himself with water in the sanctuary area and put on his regular garments. Then he shall come out and sacrifice the burnt offering for himself and the burnt offering for the people, to make atonement for himself and for the people. 25 He shall also burn the fat of the sin offering on the altar.

26 “The man who releases the goat as a scapegoat must wash his clothes and bathe himself with water; afterward he may come into the camp.27 The bull and the goat for the sin offerings, whose blood was brought into the Most Holy Place to make atonement, must be taken outside the camp; their hides, flesh and intestines are to be burned up. 28 The man who burns them must wash his clothes and bathe himself with water; afterward he may come into the camp.

God is Holy and He hates sin. People are sinful. All of us are sinners. The ceremonies which we read about above were commanded by God as a way to atone for the sins of the people. They are like a picture of what was to come. Jesus Christ Himself, God’s son came to earth as  human being. He Himself died on the cross.  As High Priest and Sacrificial Lamb Jesus atoned once and for all for the sins of all people.

Praise that Lord that we can be forgiven and we can be reconciled to God through the death and resurrection of Jesus Christ. 

JUMANNE TAREHE 20 MACHI 2018 ASUBUHI                     

WALAWI 16:20-28

20 Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai. 
21 Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. 
22 Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani. 
23 Na Haruni ataingia katika hema ya kukutania, naye atavua mavazi yake ya kitani, aliyoyavaa alipoingia katika patakatifu, atayaacha humo; 
24 naye ataosha mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na kuvaa nguo zake, na kutoka, na kusongeza sadaka ya kuteketezwa yake mwenyewe, na sadaka ya kuteketezwa ya watu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake, na kwa ajili ya watu. 
25 Na mafuta ya sadaka ya dhambi atayateketeza juu ya madhabahu. 
26 Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika marago. 
27 Na yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya marago; nao watachoma moto ngozi zao, na nyama yao, na mavi yao. 
28 Na yeye awachomaye moto atafua nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia maragoni. 

Hapo juu ni maelezo ya maagizo ya Mungu. Ni utaratibu kwa ajili ya binadamu kuomba msamaha kwa Mungu.  Mungu ni mtakatifu na binadamu wote ni wenye dhambi. Mungu aliagiza ibada hizi zifanyike ili upatanisho upatikane kati ya Mungu na binadamu.

Utaratibu huu ni kama kivuli ya yale yaliyotokea baadaye, Yesu Kristo Mwana wa Mungu alivaa ubinadamu. Yesu kama Kuhani Mkuu na kama Mwana Kondoo, alijitoa kufa msalabani. Alikufa kwa ajili ya dhambi za watu wote na alifufuka tena. Yesu alileta upatanishi kati ya Mungu na binadamu. Tumshukuru na tumwamini.