Kwaya ya Taarumbeta ya Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront ikutumbuiza katika moja ya ibada za Jumapili hapa usharikani.

Kwaya ya Tarumbeta ya Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront ni moja ya kwaya zinazofanya vizuri katika usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront. Kwaya hiyo kongwe hutumbuiza katika kila ibada ya kwanza siku za Jumapili hapa Usharikani. 

Kwaya ya Tarumbeta pia hufanya ziara za huduma katika mitaa inayotunzwa na Usharika wa Kanisa Kuu, pia hushirki katika shughuli nyingine za kijamii zinazoratibiwa na usharika.