KWAYA KUU – Kwaya ya Usharika Kanisa Kuu Azania Front (Azania Front Cathedral) ikiwa chini ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), ni Kwaya kongwe katika kwaya kuu nyingi za Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Kwaya kuu ilianza zaidi ya miaka 60 iliyopita. Hadi sasa inawaimbaji 60 waliojiandikisha, ingawaje mahudhurio ya kila ibada ni 30-40.

Kwaya hii ni miongoni mwa vikundi vinavyofanya vizuri hadi sasa katika matukio mbalimbali ya Usharika, na matukio ya DMP kwa ujumla.

Katika matukio makuu yaliyoleta historia au kujulikana kwa kwaya hii, ni uimbaji wao wa kuimba kwa kinanda au kuimba bila vyombo kwa utaalamu.

1. Kwaya Kuu imeweza kufanya vizuri katika uimbaji wa ngazi mbalimbali miaka ya nyuma (kati ya 1974 – 1995) ikiongozwa/kufundishwa na walimu mahiri. Baadhi ya majina ya walimu ambao hawatasahaulika katika historia ya Kwaya Kuu ni kama ifuatavyo:-
•Mwl Warehema Jengo (Marehemu)
•Mwl Loti Philipo Dyauli (Marehemu)
•Mwl Gideon Chaguza (Marehemu)
•Mwl Gideon Mdegela (Marehemu)
•Mwl Shekitomo
•Mwl Aminiel Mkichwe  
Mzee Marealle akiwa mmoja ya Walezi 1980 akishikilia kombe la Ushindi.

2. Kwaya Kuu imeendelea kutoa huduma za ibada zinazobariki Viongozi wa ngazi zote za DMP;

3. Mwaka wa 1980 Kwaya Kuu ilialikwa kwenda Jimbo la Bavaria Ujerumani ikiwakilisha kwaya za KKKT katika maadhimisho ya miaka 450 ya kuanzishwa kwa Kanisa la Kilutheri duniani. Maadhimisho hayo yalifanyika katika mji wa Augusburg. Kwaya iliwakilishwa na waimbaji 26 wakiongozwa na Mchungaji Bavu kutoka DMP, Mzee Eliad Simbeye ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kwaya na walimu Mzee Warehema Jengo na Mzee Loti Philipo Dyauli;

4. Ilialikwa tena na Usharika marafiki Marekani mwaka 2008;

5. Ilifanya matamasha Bagamoyo na wanakwaya waliotokea Norway 2011 kuleta mahusioano katika nchi hizi mbili.

6. Ilipata tuzo mwaka 2010 kwa ajili ya uimbaji mzuri kwa nyimbo za muziki sanifu.

7. Ushirikiano na Kwaya zingine. Kwaya kuu inashirikiana na kwaya zingine kikamilifu, Matamasha mengi, mashindano, Kantante na safari za kuwakilisha Dayosisi na Usharika kwa ujumla;

8. Kwaya kuu Azania Front ilitembelea Bukoba na kufanya tamasha la Kristmas 2010 katika Kanisa Kuu la Bukoba Mjini.

9. Kwaya Kuu iliwakilisha Usharika marafiki wa Ujerumani 2007 Usharika wa Fröndenberg, ilifanya matamasha, ilitembelea mashule, ilitembelea magereza na hospital.

Kwaya ya Pamoja ilitembelea Usharikia marafiki wa Fröndenberg Jimbo la Unna

Mipango ya katika mwaka 2012

(1)KUHUDUMIA IBADA

Kuwa na uimbaji mzuri zaidi kwa mwaka mzima;
Kwaya Kuu itaendelea kutimiza wajibu wa Kwaya kwa kuhudumu kwa njia ya uimbaji, kwa kufuata majira ya kanisa na liturgia kwa ujumla (Kalenda ya KKKT);
Kwaya Kuu itahudumia katika ibada zote za jumapili kadri Mungu atakavyowajalia; Kwaya Kuu itaendelea kutoa faraja kwa wagonjwa;
Kwaya Kuu itaendeleza huduma za ibada na kutoa faraja kwenye misiba (hasa iliyohusu wanakwaya na washarika kwa ujumla);
Kwaya Kuu itafanya Semina kwa ajili ya viongozi wa kwaya na wanakwaya kwa ujumla
Kwa Kuu itaendeleza ushirikiano katika ngazi ya Dayosisi na Usharika mzima;
 Kwa Kuu itaendeleza ushirikiano na makanisa yaliyomo nje ya dayosisi yetu yaani Tanzania na Nje ya Tanzania (Ushirikiano wa Kimataifa)

(2) MENGINEYO

Kwaya Kuu inafanya mazoezi mara tatu kwa wiki, yaani JUMANNE, JUMATANO NA IJUMAA.
Walimu
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi kubwa ambayo Mwenyenzi Mungu ametukirimia, tuna bahati ya kuwa Walimu wa kutosha wanasaidiana kusogeza mbele kazi ya Bwana.
Mwalimu wetu Mkuu ni Mwalimu Abisai Faragha
Mwalimu Amri Pangapanga Hingi
Mwalimu Godfrey Moshi.

Tuna kila sababu za kutosha za Kumshukuru Mungu kwa ajili ya Walimu wetu.

(3) HITIMISHO

Tutaendeleza ushirikiano kwa Viongozi wa juu wa Dayosisi, Usharikani na vikundi vyote kwa ujumla.

Kwa Ushirikiano imetolewa: KWAYA KUU AZANIA FRONT

Group Articles

No articles yet!