Date: 
04-10-2021
Reading: 
Kumbukumbu la Torati 6:20-25 (Deuteronomy)

JUMATATU TAREHE 4 OKTOBA 2021, ASUBUHI

Kumbukumbu la Torati 6:20-25

20 Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, N’nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu?

21 Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu;

22 BWANA akaonya ishara na maajabu, makubwa, mazito, juu ya Misri, na juu ya Farao, na juu ya nyumba yake yote, mbele ya macho yetu;

23 akatutoa huko ili kututia huku, apate kutupa nchi aliyowaapia baba zetu.

24 BWANA akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche BWANA, Mungu wetu, tuone mema sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo.

25 Tena itakuwa haki kwetu, tukitunza kufanya maagizo haya yote mbele ya BWANA, Mungu wetu, kama alivyotuagiza.

 

Tuwapende na kuwajali watoto;

Israeli wanaagizwa kuwafundisha watoto wao juu ya nguvu ya Mungu kwao, na upendo wake, kwa jinsi alivyowaokoa toka utumwani. Bwana anawataka Israeli kuwafundisha watoto wao juu ya amri zake, ili wazidi katika kumwamini na kumtumikia yeye.

Ndivyo Mungu anavyotutaka kufundisha na kuhubiri kwa watu wote juu ya nguvu yake na wokovu wake, ya kuwa yeye ndiye mkombozi wa ulimwengu. Anatutaka kuhubiri kuwa, yeye ndiye BWANA aokoaye, anayestahili kuabudiwa na ulimwengu wote.

Ni wajibu wetu kuhubiri habari njema ya wokovu kwa watu wote, ili imani hii ya kweli katika Yesu Kristo idumu na kukua, Kanisa lake likikua na kuongezeka katika kuueneza ufalme wake ili watu wote waokolewe na kumtumikia yeye.

Uwe na wiki njema yenye baraka na mafanikio.


MONDAY 4TH OCTOBER 2021, MORNING

Deuteronomy 6:20-25

20 “When your son asks you in time to come, ‘What is the meaning of the testimonies and the statutes and the rules that the Lord our God has commanded you?’ 21 then you shall say to your son, ‘We were Pharaoh's slaves in Egypt. And the Lord brought us out of Egypt with a mighty hand. 22 And the Lord showed signs and wonders, great and grievous, against Egypt and against Pharaoh and all his household, before our eyes. 23 And he brought us out from there, that he might bring us in and give us the land that he swore to give to our fathers. 24 And the Lord commanded us to do all these statutes, to fear the Lord our God, for our good always, that he might preserve us alive, as we are this day. 25 And it will be righteousness for us, if we are careful to do all this commandment before the Lord our God, as he has commanded us.’

Let us love and care for children;

Israel is commanded to teach their children about God's power for them, and His love, for how He delivered them from bondage. The Lord wants Israel to teach their children about His commandments, so that they may grow in faith and service to Him.

That is how God wants us to teach and preach to all people about His power and salvation, that He is the Redeemer of the world. He wants us to preach that He is the saving Lord, worthy of all the worship of the world.

It is our responsibility to preach the good news of salvation to all people, so that this true faith in Jesus Christ may continue and grow, as His Church grows and expands in spreading His kingdom so that all people may be saved and serve Him.

Have a wonderful week with blessings and success.