Date: 
04-05-2020
Reading: 
Joshua 6:12-20

MONDAY 4TH MAY 2020  MORNING                                                                     

Joshua 6:12-20 New International Version (NIV)

12 Joshua got up early the next morning and the priests took up the ark of the Lord. 13 The seven priests carrying the seven trumpets went forward, marching before the ark of the Lord and blowing the trumpets. The armed men went ahead of them and the rear guard followed the ark of the Lord, while the trumpets kept sounding. 14 So on the second day they marched around the city once and returned to the camp. They did this for six days.

15 On the seventh day, they got up at daybreak and marched around the city seven times in the same manner, except that on that day they circled the city seven times. 16 The seventh time around, when the priests sounded the trumpet blast, Joshua commanded the army, “Shout! For the Lord has given you the city! 17 The city and all that is in it are to be devoted[a] to the Lord. Only Rahab the prostitute and all who are with her in her house shall be spared, because she hid the spies we sent. 18 But keep away from the devoted things, so that you will not bring about your own destruction by taking any of them. Otherwise you will make the camp of Israel liable to destruction and bring trouble on it. 19 All the silver and gold and the articles of bronze and iron are sacred to the Lord and must go into his treasury.”

20 When the trumpets sounded, the army shouted, and at the sound of the trumpet, when the men gave a loud shout, the wall collapsed; so everyone charged straight in, and they took the city. 

Israel's problem was that they had a city to conquer, but there were huge walls surrounding the city.

 As we go through life, we have obstacles that we face as well.

Here, God promises Israel the victory before they ever attack Jericho.

As we face life obstacles, whatever they may be we can do so with confidence, because we have the Lord's promises that we can do all things through Christ who strengthens us.


JUMATATU TAREHE 4 MEI 2020   ASUBUHI                                                           

YOSHUA 6:12-20

12 Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao makuhani wakalichukua sanduku la Bwana.
13 Na wale makuhani saba wakazichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana, wakaendelea wakazipiga tarumbeta; nao watu wenye silaha wakawatangulia, na hao waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la Bwana; makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda.
14 Siku ya pili wakauzunguka mji mara moja, wakarejea kambini; ndivyo walivyofanya siku sita.
15 Ikawa siku ya saba wakaondoka asubuhi na mapema wakati wa mapambazuko, wakauzunguka mji vivyo hivyo mara saba; ila siku hiyo waliuzunguka huo mji mara saba.
16 Hata mara ya saba makuhani walipozipiga tarumbeta, Yoshua akawaambia watu, Pigeni kelele; kwa maana Bwana amewapeni mji huu.
17 Na mji huu utakuwa wakfu kwa Bwana, mji wenyewe na vitu vyote vilivyomo; isipokuwa Rahabu, yule kahaba, ataishi, yeye na watu wote walio pamoja naye nyumbani, kwa sababu aliwaficha hao wapelelezi tuliowatuma.
18 Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtayafanya matuo ya Israeli kuwa yamelaaniwa na kuyafadhaisha.
19 Lakini fedha yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na chuma, ni vitakatifu kwa Bwana; vitaletwa katika hazina ya Bwana.
20 Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili mbele; wakautwaa huo mji.

Hitaji au tatizo kubwa la Israeli lilikuwa kuuteka mji, lakini mbele yao kulikuwa na kuta kubwa zilizouzunguka mji. 

 Kila mara katika maisha yetu tunakutana na vikwazo vingi.    

Hapa, tunaona Mungu akiwaahidi Waisraeli ushindi hata kabla ya kuukabili mji wa Yeriko. 

Tunapokutana na vikwazo maishani mwetu, kwa hali yoyote ile, tunao ujasiri  kwa maana tunayo ahadi ya Bwana kuwa “Tunayaweza mambo yote katika Kristo atutiaye nguvu.”