Date: 
27-01-2018
Reading: 
John 7:14-24 NIV (Yohana 7:14-24)

SATURDAY  27TH JANUARY 2018 MORNING                              

John 7:14-24 New International Version (NIV)

Jesus Teaches at the Festival

14 Not until halfway through the festival did Jesus go up to the temple courts and begin to teach. 15 The Jews there were amazed and asked, “How did this man get such learning without having been taught?”

16 Jesus answered, “My teaching is not my own. It comes from the one who sent me. 17 Anyone who chooses to do the will of God will find out whether my teaching comes from God or whether I speak on my own.18 Whoever speaks on their own does so to gain personal glory, but he who seeks the glory of the one who sent him is a man of truth; there is nothing false about him. 19 Has not Moses given you the law? Yet not one of you keeps the law. Why are you trying to kill me?”

20 “You are demon-possessed,” the crowd answered. “Who is trying to kill you?”

21 Jesus said to them, “I did one miracle, and you are all amazed. 22 Yet, because Moses gave you circumcision (though actually it did not come from Moses, but from the patriarchs), you circumcise a boy on the Sabbath. 23 Now if a boy can be circumcised on the Sabbath so that the law of Moses may not be broken, why are you angry with me for healing a man’s whole body on the Sabbath? 24 Stop judging by mere appearances, but instead judge correctly.”

Notice what Jesus says in verse 11. Do we really want to  know the truth? The Jewish leaders and many of the ordinary Jews did not want to accept Jesus’s teachings. They closed their minds. May God help us to keep listening both with our outward ears and with our spiritual ears. May God help us to hear and understand and believe the truth and to live it out in our lives.   

JUMAMOSI TAREHE 27 JANUARI 2018 ASUBUHI                               

YOHANA 7:14-24

14 Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alikwea kuingia hekaluni, akafundisha. 
15 Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma? 
16 Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. 
17 Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. 
18 Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu. 
19 Je! Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua? 
20 Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua? 
21 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnaistaajabia. 
22 Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi siku ya sabato humtahiri mtu. 
23 Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? 
24 Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki. 
 

Tazama jinsi Yesu alisema  katika mstari wa 11. Viongozi wa Wayahudi na Wayahudi wengi wa kawaida hawakutaka kusikia  ukweli.   Wayahudi hawakutaka kusikiliza mafundisho ya Yesu. Mungu atusaidie kusikiliza kwa maskio ya kawaida na ya kiroho. Tukiamini ukweli kuhusu Yesu na kuzingatia katika maisha yetu.