Date: 
25-10-2019
Reading: 
John 4:46-54 

FRIDAY 25TH OCTOBER 2019 MORNING  

John 4:46-54 New International Version (NIV)

46 Once more he visited Cana in Galilee, where he had turned the water into wine. And there was a certain royal official whose son lay sick at Capernaum. 47 When this man heard that Jesus had arrived in Galilee from Judea, he went to him and begged him to come and heal his son, who was close to death.

48 “Unless you people see signs and wonders,” Jesus told him, “you will never believe.”

49 The royal official said, “Sir, come down before my child dies.”

50 “Go,” Jesus replied, “your son will live.”

The man took Jesus at his word and departed. 51 While he was still on the way, his servants met him with the news that his boy was living. 52 When he inquired as to the time when his son got better, they said to him, “Yesterday, at one in the afternoon, the fever left him.”

53 Then the father realized that this was the exact time at which Jesus had said to him, “Your son will live.” So he and his whole household believed.

54 This was the second sign Jesus performed after coming from Judea to Galilee.

Sometimes we miss out on the blessings of God because we wait and look for the evidence before we will believe. The royal official believed and experienced God at work in his life. Neither distance, nor time has any negative factor when God is at work.


IJUMAA TAREHE 25 OKTOBA 2019 ASUBUHI 

YOHANA 4:46-54

46 Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu.
47 Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani.
48 Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa?
49 Yule diwani akamwambia, Bwana, ushuke asijakufa mtoto wangu.
50 Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia.
51 Hata alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu hai.
52 Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha.
53 Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake.
54 Hiyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Uyahudi kufika Galilaya.

 

Wakati mwingine tunazikosa Baraka za Mungu kwa sababu tunasubiri tuone matendo ya Mungu ndipo tuamini.  Diwani huyu aliamini, naye akaaona matendo makuu ya Mungu katika maisha yake. Mungu anapoamua kuitenda kazi yake, hawezi kuzuiwa na muda wala umbali.