Date: 
30-10-2019
Reading: 
John 2:13-22 (Yohana 2:13-22)

WEDNESDAY 30TH OCTOBER 2019 MORNING   

John 2:13-22 New International Version (NIV)

13 When it was almost time for the Jewish Passover, Jesus went up to Jerusalem. 14 In the temple courts he found people selling cattle, sheep and doves, and others sitting at tables exchanging money. 15 So he made a whip out of cords, and drove all from the temple courts, both sheep and cattle; he scattered the coins of the money changers and overturned their tables. 16 To those who sold doves he said, “Get these out of here! Stop turning my Father’s house into a market!” 17 His disciples remembered that it is written: “Zeal for your house will consume me.”[c]

18 The Jews then responded to him, “What sign can you show us to prove your authority to do all this?”

19 Jesus answered them, “Destroy this temple, and I will raise it again in three days.”

20 They replied, “It has taken forty-six years to build this temple, and you are going to raise it in three days?” 21 But the temple he had spoken of was his body. 22 After he was raised from the dead, his disciples recalled what he had said. Then they believed the scripture and the words that Jesus had spoken.

 

Lesson 1

The Temple represented the location and the presence of God. Jesus declared that a new Temple would be found in his own resurrected body. Instead of God’s presence being confined to a single geographical site, God will be everywhere; and we are the temple of God in the world.

May we too, like the disciples, understand these words of Jesus and believe them.

Lesson 2

When you see things going on which are wrong, do you do anything about it? We need to ask Jesus Christ for courage to stand up for the truth and not to give in to those who threaten us.


JUMATANO TAREHE 30 OKTOBA 2019 ASUBUHI                                           

YOHANA 2:13-22

13 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.
14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.
15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;
16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.
17 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.
18 Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya?
19 Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.
20 Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?
21 Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.
22 Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.

Hekalu liliwakilisha mahali na uwepo wa Mungu. Yesu Kristo anatangaza kwamba yeye ndiye hakalu jipya baada ya ufufuko wake. Badala ya uwepo wa Mungu kuwa katika eneo moja, sasa Mungu atapatikana mahali pote; na sisi Wakristo ni hekalu lake Mungu hapa duniani.

Tumwombe Mungu atujalie, kama wale mitume, tupate kuelewa haya maneno ya Yesu na kuyaamini.

**********************           ***********************        

Je, unapoona mambo mabaya yanatendeka, unachukua hatua yoyote? Tumwombe Yesu Kristo, atupe ujasiri wa kusimamia kweli, na kamwe tusirudi nyuma hata kwa sababu ya vitisho.