Date: 
07-04-2018
Reading: 
John 20:11-18 (Yohana 20:11-18)

SATURDAY   7TH APRIL 2018 MORNING                            


John 20:11-18 New International Version (NIV)


Jesus Appears to Mary Magdalene


11 Now Mary stood outside the tomb crying. As she wept, she bent over to look into the tomb 12 and saw two angels in white, seated where Jesus’ body had been, one at the head and the other at the foot.
13 They asked her, “Woman, why are you crying?”
“They have taken my Lord away,” she said, “and I don’t know where they have put him.” 14 At this, she turned around and saw Jesus standing there, but she did not realize that it was Jesus.
15 He asked her, “Woman, why are you crying? Who is it you are looking for?”
Thinking he was the gardener, she said, “Sir, if you have carried him away, tell me where you have put him, and I will get him.”
16 Jesus said to her, “Mary.”
She turned toward him and cried out in Aramaic, “Rabboni!” (which means “Teacher”).
17 Jesus said, “Do not hold on to me, for I have not yet ascended to the Father. Go instead to my brothers and tell them, ‘I am ascending to my Father and your Father, to my God and your God.’”
18 Mary Magdalene went to the disciples with the news: “I have seen the Lord!” And she told them that he had said these things to her.


The above passage is part of the Apostle John’s description of what happened on Easter Sunday when Jesus rose from the dead.  Mary did not recognize Jesus at first but when He spoke her name she knew it was her Lord Jesus.  Mary was amazed and delighted to see the risen Lord Jesus.
Have you heard Jesus calling your name? Are you walking with and talking to the Risen Lord Jesus day by day?


JUMAMOSI  TAREHE 7 APRILI 2018  ASUBUHI                          

YOHANA 20:11-18

11 Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. 
12 Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu. 
13 Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka. 
14 Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. 
15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. 
16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu). 
17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. 
18 Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo. 

Maneno hapo juu ni sehemu ya maelezo ya Mtume Yohana kuhusu siku ya Jumapili ya Pasaka. Mwanzoni Mariamu hakumtambua Bwana Yesu lakini baada ya Yesu kutamka jina lake amemtambu. Mariamu alifurahi sana kumwona Bwana Wake Yesu Kristo aliyefufuka.
Je! Unamsikia Bwana Yesu akiita jina lako? Unatembea naye na Kuongea kila siku na Bwana Yesu aliyefufuka ?