Date: 
29-05-2020
Reading: 
John 15:18-25 (Yohana 15:18-25)

FRIDAY 29TH MAY 2020    MORNING                                                            

John 15:18-25 New International Version (NIV)

18 “If the world hates you, keep in mind that it hated me first. 19 If you belonged to the world, it would love you as its own. As it is, you do not belong to the world, but I have chosen you out of the world. That is why the world hates you. 20 Remember what I told you: ‘A servant is not greater than his master.’[b] If they persecuted me, they will persecute you also. If they obeyed my teaching, they will obey yours also. 21 They will treat you this way because of my name, for they do not know the one who sent me. 22 If I had not come and spoken to them, they would not be guilty of sin; but now they have no excuse for their sin. 23 Whoever hates me hates my Father as well. 24 If I had not done among them the works no one else did, they would not be guilty of sin. As it is, they have seen, and yet they have hated both me and my Father. 25 But this is to fulfill what is written in their Law: ‘They hated me without reason.

If you live in obedience to Jesus Christ, you will threaten unbelievers in your family, at school, or at work, because your godly life will expose their sin. As a result, they will attack you falsely. But in spite of the world’s hatred, we should never respond with retaliation or hatred.


IJUMAA TAREHE 29 MEI 2020    ASUBUHI                                         

YOHANA 15:18-25

18 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.
19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
20 Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.
21 Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka.
22 Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.
23 Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu.
24 Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.
25 Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure.

Ikiwa unaishi kwa kumtii Yesu Kristo, utakuwa ni tishio kwa wasioamini, familia yako, shuleni au kazini kwako, kwa sababu maisha yako ya Kikristo yatadhihirisha dhambi zao. Kwa sababu hiyo, watakushambulia kwa mambo ya kusingiziwa. Lakini pamoja na kuchukiwa na ulimwengu huu, tusilipize kwa mabaya au kwa chuki.