Date: 
23-02-2017
Reading: 
Jeremiah 45 (NIV)

THURSDAY 23RD FEBRUARY 2017 MORNING                               

Jeremiah 45 New International Version (NIV)

A Message to Baruch

1 When Baruch son of Neriah wrote on a scroll the words Jeremiah the prophet dictated in the fourth year of Jehoiakim son of Josiah king of Judah, Jeremiah said this to Baruch: “This is what the Lord, the God of Israel, says to you, Baruch: You said, ‘Woe to me! The Lord has added sorrow to my pain; I am worn out with groaning and find no rest.’ But the Lord has told me to say to you, ‘This is what the Lord says: I will overthrow what I have built and uproot what I have planted, throughout the earth. Should you then seek great things for yourself? Do not seek them. For I will bring disaster on all people, declares the Lord, but wherever you go I will let you escape with your life.’”

Jeremiah was a prophet called by God to speak His words to people. This is one of the messages from God. Here we hear a special message for Baruch.  God also wants to speak His Word to you. When you read His Word in the Bible and when you pray ask God to speak to you personally. Ask God to be with you and guide you in the challenges you face in your life.

ALHAMISI TAREHE 23 FEBRUARI  2017 ASUBUHI                            

YEREMIA 45:1-5

1Neno hili ndilo ambalo Yeremia, nabii, alimwambia Baruku, mwana wa Neria, alipoyaandika maneno haya katika kitabu kwa kinywa cha Yeremia, mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kusema, 
2 Bwana, Mungu wa Israeli, akuambia wewe Ee Baruku; 
3 Ulisema, Ole wangu! Kwa maana Bwana ameongeza huzuni pamoja na maumivu yangu. Nimechoka kwa ajili ya kuugua kwangu, wala sioni raha. 
4 Basi, mwambie hivi, Bwana asema hivi, Tazama, niliyoyajenga nitayabomoa, na niliyoyapanda nitayang'oa; na haya yatakuwa katika nchi yote. 
5 Je! Unajitafutia mambo makuu? Usiyatafute; kwa maana tazama, nitaleta mabaya juu ya wote wenye mwili, asema Bwana; lakini roho yako nitakupa iwe nyara, katika mahali pote utakapokwenda.

Yeremia alikuwa Nabii aliyeitwa na Mungu. Aliitwa kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu mbalimbali. Hapo juu tumesoma ujumbe wa Mungu kwa Baruku. Mungu anataka kuongea na wewe pia. Wakati unasoma Biblia na wakati wa maombi, umwombe Mungu akupe Neno kwa nasfi yako. Mwombe Mungu akuongoze na kukutia nguvu katika changamoto za maisha yako.