Date: 
22-08-2017
Reading: 
Jeremiah 3:21-25 NIV ( Yeremia 3:21-25)

TUESDAY 22ND AUGUST 2017   MORNING                                    

Jeremiah 3:21-25  New International Version (NIV)

21 A cry is heard on the barren heights,
    the weeping and pleading of the people of Israel,
because they have perverted their ways
    and have forgotten the Lord their God.

22 “Return, faithless people;
    I will cure you of backsliding.”

“Yes, we will come to you,
    for you are the Lord our God.
23 Surely the idolatrous commotion on the hills
    and mountains is a deception;
surely in the Lord our God
    is the salvation of Israel.
24 From our youth shameful gods have consumed
    the fruits of our ancestors’ labor—
their flocks and herds,
    their sons and daughters.
25 Let us lie down in our shame,
    and let our disgrace cover us.
We have sinned against the Lord our God,
    both we and our ancestors;
from our youth till this day
    we have not obeyed the Lord our God.”

The words of the Prophet Jeremiah recorded above contain both a message from God in verse 22 calling the people to come back to the true God. Then the people respond by admitting their sins.

Let us listen to God today. Perhaps we need to change our lives. Let us pray that God will forgive our sins and cleanse us from all unrighteousness.

JUMANNE TAREHE 22 AGOSTI 2017 ASUBUHI                                      

YEREMIA 3:21-25

21 Sauti inasikiwa juu ya vilele vya milima, ni kulia kwao na maombi yao wana wa Israeli; kwa kuwa wameipotosha njia yao, wamemsahau Bwana, Mungu wao. 
22 Rudini, enyi watoto waasi, mimi nitaponya maasi yenu. Tazama, tumekuja kwako; maana wewe u Bwana, Mungu wetu. 
23 Ni kweli, msaada haufai unaotazamiwa kutoka milimani, makutano yenye mshindo juu ya milima; ni kweli, wokovu wa Israeli ni katika Bwana, Mungu wetu. 
24 Lakini kitu cha aibu kimeila kazi ya baba zetu tokea ujana wetu; makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao. 
25 Na tulale kwa aibu yetu, haya yetu na itufunike; kwa maana tumemwasi Bwana, Mungu wetu, sisi na baba zetu, tangu ujana wetu hata leo; wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu.

Katika maneno ya Nabii Yeremia yaliyoandikwa hapa juu tunasikia sauti ya Mungu akiita watu kutubu na kurejea kwake ( mst 22). Pia tunasikia watu kukubali kwamba ni wenye dhambi na walimwaasi Mungu na kukubali kutubu.

Je! Tumesikia sauti ya Mungu leo? Anatuambia tuchunguze mwenendo wetu na tumwombe atusamahehe na kutusafisha.