Date: 
28-01-2017
Reading: 
James 2:1-7 (NIV)

 SATURDAY 28TH JANUARY 2017 MORNING                                   

James 2:1-7  New International Version (NIV)

Favoritism Forbidden

1 My brothers and sisters, believers in our glorious Lord Jesus Christ must not show favoritism. Suppose a man comes into your meeting wearing a gold ring and fine clothes, and a poor man in filthy old clothes also comes in. If you show special attention to the man wearing fine clothes and say, “Here’s a good seat for you,” but say to the poor man, “You stand there” or “Sit on the floor by my feet,” have you not discriminated among yourselves and become judges with evil thoughts?

Listen, my dear brothers and sisters: Has not God chosen those who are poor in the eyes of the world to be rich in faith and to inherit the kingdom he promised those who love him? But you have dishonored the poor. Is it not the rich who are exploiting you? Are they not the ones who are dragging you into court? Are they not the ones who are blaspheming the noble name of him to whom you belong?

This is a challenge to us. Do we show favoritism in our churches? Do we show favoritism in other areas of our life?

We often look on the outward appearance but God sees what is in a person’s heart.  May God help us not to judge people unfairly but to show consideration and respect to each person we meet.

 

JUMAMOSI TAREHE 28 JANUARI 2017 ASUBUHI                            

YAKOBO 2:1-7

1 Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu. 
2 Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; 
3 nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, 
4 je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? 
5 Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? 
6 Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! Matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu? 
7 Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa? 

Maneno haya ni changamoto kwetu. Je! Tunaonyesha upendeleo kanisani au mahali pengine? Tunabagua na kudharau wengine na kuheshimu wengine? Mara nyingi tunajali yaliyonekana nje bila kujua ya ndani ya mtu. Mungu huangalia moyo ya mtu. Tumwombee Mungu atuwezeshe kuheshimu na kujali kila mtu.