Date: 
07-01-2022
Reading: 
Isaya 2:2-5

Ijumaa asubuhi tarehe 07.01.2021

Isaya 2:2-5

2 Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.

3 Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.

4 Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.

5 Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.

Waliomngojea Mwokozi wamuona;

Nabii Isaya anatoa utabiri unaohusu Bwana kulijia Taifa lake, baada ya tabu za dunia kuisha. Ni wakati ambao watu wote watamtafuta Bwana, maana ujio wake hauepukiki. Isaya anaendelea kusema kuwa Bwana atarudi kwa hukumu kwa mataifa, anamalizia kwa kuwaita watu wa Yerusalemu kumrudia Bwana.

Sauti hii ya Isaya iliyowaita Israeli, inatuita leo kumrudia Bwana, tukijiandaa na ujio wake. Ni vema tuwe katika njia sahihi, ili tuwe na uhakika wa kumlaki Bwana. Tuendelee kumngoja, tutamuona.

Siku njema.