Date: 
07-12-2020
Reading: 
Isaiah 59:16-21

MONDAY 7TH DECEMBER 2020 MORNING                                                                      

Isaiah 59:16-21New International Version (NIV)

16 He saw that there was no one,
    he was appalled that there was no one to intervene;
so his own arm achieved salvation for him,
    and his own righteousness sustained him.
17 He put on righteousness as his breastplate,
    and the helmet of salvation on his head;
he put on the garments of vengeance
    and wrapped himself in zeal as in a cloak.
18 According to what they have done,
    so will he repay
wrath to his enemies
    and retribution to his foes;
    he will repay the islands their due.
19 From the west, people will fear the name of the Lord,
    and from the rising of the sun, they will revere his glory.
For he will come like a pent-up flood
    that the breath of the Lord drives along.[a]

20 “The Redeemer will come to Zion,
    to those in Jacob who repent of their sins,”
declares the Lord.

21 “As for me, this is my covenant with them,” says the Lord. “My Spirit, who is on you, will not depart from you, and my words that I have put in your mouth will always be on your lips, on the lips of your children and on the lips of their descendants—from this time on and forever,” says the Lord.

God is teaching us that no man can redeem him/herself. There is no human cure for what our world is going through right now. Jesus is the only answer to our problems.


JUMATATU TAREHE 7 DESEMBA 2020 ASUBUHI                                          

ISAYA 59:16-21

16 Akaona ya kuwa hapana mtu, akastaajabu kwa kuwa hapana mwombezi; basi, mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu; na haki yake ndiyo iliyomsaidia.
17 Akajivika haki kama deraya kifuani, na chapeo cha wokovu kichwani pake, akajivika mavazi ya kisasi yawe mavazi yake, naye alivikwa wivu kama joho.
18 Kadiri ya matendo yao, kwa kadiri iyo hiyo atawalipa, ukali kwao wampingao, malipo kwa adui zake; naye atavirudishia visiwa malipo.
19 Basi, wataliogopa jina la Bwana toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya Bwana.
20 Na Mkombozi atakuja Sayuni, kwao waachao maasi yao katika Yakobo, asema Bwana.
21 Tena katika habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema Bwana; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema Bwana, tangu leo na hata milele.

Mungu anatufundisha kuwa, hakuna mwanadamu awezaye kujiokoa mwenyewe. Hakuna tiba yoyote ya kibinadamu kwa ajili ya hali dunia yetu inayopitia kwa sasa. Yesu ndilo jibu pekee la matatizo yetu.