Date: 
05-05-2020
Reading: 
Isaiah 38:9-15

TUESDAY 5TH MAY 2020  MORNING                                                   

Isaiah 38:9-15 The New International Version (NIV)

A writing of Hezekiah king of Judah after his illness and recovery:

10 I said, “In the prime of my life
    must I go through the gates of death
    and be robbed of the rest of my years?”
11 I said, “I will not again see the Lord himself
    in the land of the living;
no longer will I look on my fellow man,
    or be with those who now dwell in this world.
12 Like a shepherd’s tent my house
    has been pulled down and taken from me.
Like a weaver I have rolled up my life,
    and he has cut me off from the loom;
    day and night you made an end of me.
13 I waited patiently till dawn,
    but like a lion he broke all my bones;
    day and night you made an end of me.
14 I cried like a swift or thrush,
    I moaned like a mourning dove.
My eyes grew weak as I looked to the heavens.
    I am being threatened; Lord, come to my aid!”

15 But what can I say?
    He has spoken to me, and he himself has done this.
I will walk humbly all my years
    because of this anguish of my soul.

The more serious our trial, the more intensely we tend to pray. Hezekiah’s experience teaches us how to conduct ourselves before the LORD in times of trials and difficulties.

As long as we have breath, we can return to the LORD just as Hezekiah did and the LORD will have mercy upon us. He will hear our prayers and meet our needs.


JUMANNE TAREHE 5 MEI 2020  ASUBUHI                                                 

ISAYA 38:9-15

Haya ndiyo maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda, alipokuwa hawezi, naye akapona ugonjwa wake.
10 Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.
11 Nalisema, Sitamwona Bwana, yeye Bwana, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.
12 Kao langu limeondolewa kabisa, limechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
13 Nalijituliza hata asubuhi; kama simba, aivunja mifupa yangu yote; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
14 Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Naliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee Bwana, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.
15 Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.

Inapotokea tukapita katika mambo magumu sana, tunazidisha bidii katika kuomba. Maisha ya Hezekia yanatufundisha jinsi ya kwenda mbele za Mungu tunapopita katika majaribu na mambo magumu.

Wakati tungali bado na uhai, tunaweza kumrudia Bwana kama alivyofanya Hezekia; na Bwana atatuhurumia. Atayasikia maombi yetu na kukutana na mahitaji yetu.