Date: 
21-04-2020
Reading: 
Isaiah 33:13-24 

TUESDAY 21ST APRIL 2020  MORNING                                                           

Isaiah 33:13-24 New International Version (NIV)

13 You who are far away, hear what I have done;
    you who are near, acknowledge my power!
14 The sinners in Zion are terrified;
    trembling grips the godless:
“Who of us can dwell with the consuming fire?
    Who of us can dwell with everlasting burning?”
15 Those who walk righteously
    and speak what is right,
who reject gain from extortion
    and keep their hands from accepting bribes,
who stop their ears against plots of murder
    and shut their eyes against contemplating evil—
16 they are the ones who will dwell on the heights,
    whose refuge will be the mountain fortress.
Their bread will be supplied,
    and water will not fail them.

17 Your eyes will see the king in his beauty
    and view a land that stretches afar.
18 In your thoughts you will ponder the former terror:
    “Where is that chief officer?
Where is the one who took the revenue?
    Where is the officer in charge of the towers?”
19 You will see those arrogant people no more,
    people whose speech is obscure,
    whose language is strange and incomprehensible.

20 Look on Zion, the city of our festivals;
    your eyes will see Jerusalem,
    a peaceful abode, a tent that will not be moved;
its stakes will never be pulled up,
    nor any of its ropes broken.
21 There the Lord will be our Mighty One.
    It will be like a place of broad rivers and streams.
No galley with oars will ride them,
    no mighty ship will sail them.
22 For the Lord is our judge,
    the Lord is our lawgiver,
the Lord is our king;
    it is he who will save us.

23 Your rigging hangs loose:
    The mast is not held secure,
    the sail is not spread.
Then an abundance of spoils will be divided
    and even the lame will carry off plunder.
24 No one living in Zion will say, “I am ill”;
    and the sins of those who dwell there will be forgiven.

Jesus paid the debt of sin for all who would believe in Him.

When Jesus forgives sin he heals sicknesses; and when the diseases of sin are removed by the mercy of forgiveness, the pain of the body is removed and its sources removed; so that his people can no longer suffer or acknowledge the presence of disease in them.


JUMANNE TAREHE 21 APRILI 2020  ASUBUHI 

ISAYA 33:13-24

13 Sikieni, ninyi mlio mbali, niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uweza wangu.
14 Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?
15 Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung'utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.
16 Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
17 Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri wake, yataona nchi iliyoenea sana.
18 Moyo wako utatafakari hofu ile; Yuko wapi yeye aliyehesabu? Yuko wapi yeye aliyeupima ushuru? Yuko wapi yeye aliyeihesabu minara?
19 Hutawaona watu wale wakali; watu wa maneno magumu usiyoweza kuyafahamu; wenye lugha ya kigeni usiyoweza kuelewa nayo.
20 Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika.
21 Bali huko Bwana atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo.
22 Kwa maana Bwana ndiye mwamuzi wetu; Bwana ndiye mfanya sheria wetu; Bwana ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.
23 Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza sana shina la mlingoti wao; hawakuweza kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka.
24 Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.

Yesu alilipa deni ya dhambi kwa ajili ya watu wote watakaomwamini.

Yesu anaposamehe dhambi anaponya na magonjwa; na magonjwa ya dhambi yanapoondolewa kwa huruma ya msamaha, maumivu ya mwili huondolewa na vyanzo vyake kutolewa; ili watu wake wasiugue tena au kukiri tena uwepo wa magonjwa kwao.