Date: 
23-05-2020
Reading: 
Hebrews 8:1-8

SATURDAY 23RD MAY 2020     MORNING                                                   

Hebrew 8:1-8  New International Version (NIV)

1 Now the main point of what we are saying is this: We do have such a high priest, who sat down at the right hand of the throne of the Majesty in heaven, 2 and who serves in the sanctuary, the true tabernacle set up by the Lord, not by a mere human being.

3 Every high priest is appointed to offer both gifts and sacrifices, and so it was necessary for this one also to have something to offer. 4 If he were on earth, he would not be a priest, for there are already priests who offer the gifts prescribed by the law. 5 They serve at a sanctuary that is a copy and shadow of what is in heaven. This is why Moses was warned when he was about to build the tabernacle: “See to it that you make everything according to the pattern shown you on the mountain.”[a] 6 But in fact the ministry Jesus has received is as superior to theirs as the covenant of which he is mediator is superior to the old one, since the new covenant is established on better promises.

7 For if there had been nothing wrong with that first covenant, no place would have been sought for another. 8 But God found fault with the people and said[b]:

“The days are coming, declares the Lord,
    when I will make a new covenant
with the people of Israel
    and with the people of Judah.

Christianity requires obedience. It is not the external obedience of rules and rituals, but obedience from the heart out of love for God.

We must daily seek to know Christ, to love Him, and to glorify Him because He gave Himself on the cross for us.

 “Therefore if you have been raised up with Christ, keep seeking the things above, where Christ is, seated at the right hand of God. Set your mind on the things above, not on the things that are on earth. For you have died and your life is hidden with Christ in God. When Christ, who is our life, is revealed, then you also will be revealed with Him in glory” (Colossians 3:1-4). 


JUMAMOSI TAREHE 23 MEI 2020 ASUBUHI                              WAEBRANIA 8:1-5

1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,
2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.
3 Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa.
4 Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria;
5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
6 Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.
7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili.
8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya;

 

Mkristo anahitaji kuwa mtiifu. Siyo utii wa nje katika kufuata sheria na taratibu, lakini ni kutii kunakotokana na kumpenda Mungu kwa moyo wote. Kila siku tunahitaji kutafuta kumjua Kristo, kumpenda, na kumtukuza kwa sababu yeye alijitoa msalabani kwa ajili yetu.

“Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristoaliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. “ (Wakolosai  3:1-4).